Home Mchanganyiko TGNP , WADAU WATOA MAONI KWA MRENGO WA KIJINSIA KUHUSU BAJETI KUU...

TGNP , WADAU WATOA MAONI KWA MRENGO WA KIJINSIA KUHUSU BAJETI KUU YA SERIKALI MWAKA 2021/22

0
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi

TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI

MAONI YA WADAU JUU YA
BAJETI KUU YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

11JUNE 2020.

Bajeti yenye Mrengo waJinsia:
Chachu ya Uchumi Jumuishi, Viwanda na Maendeleo ya Watu

Mtandao
wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa kushirikiana na wadau kutoka asasi za kiraia na vikundi
vya kijamii kutoka mikoa mbalimbali nchini tulipata fursa mnamo tarehe 10 Juni
mwaka huu, kupitia mjadala wa Bajeti ya Taifa,kufuatilia kwa pamoja na
kuchambuabajeti ya mwaka wa fedha 2020/21 iliyokuwa ikiwasilishwa bungeni na
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba (MB) na baadae kutoa
maoni yetu juu ya bajeti hiyo iliyotanguliwa na hotuba ya Hali Halisi ya Uchumi
wa Tanzania.

Kama
inavyojulikana, Bajeti kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inatoa mwelekeo wa mipango ya maendeleo kwa kila sekta kwa mwaka unaohusika.
Bajeti Kuu ya Serikali ni kielelezo cha jinsi gani Serikali Kuu ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania imejipanga na kupendekeza mwelekeo wa namna afua zilizopendekezwa
katika sekta mbalimbali zitagharamiwa ili kuleta mabadiliko katika nchi kwa
mwaka husika. Hivyo basi, Bajeti Kuu ya Serikali ni kielelezo kikubwa na muhimu
sana katika kuashiria jinsi Serikali Kuu inapendekeza kuletea wananchi wake
maendeleo kulingana na mahitaji au malengo ya kitaifa.

Bajeti
hii ni ya kwanza chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Rais wa kwanza Mwanamke nchini na ukanda wa Afrika Mashariki, ambaye ametamka
wazi katika hotuba zake mbalimbali kuwa masualaya usawa wa kijinsia ni kapaumbele
chake kikubwa miongoni mwa vipaumbele vya Serikali yake ya Awamu ya Sita. Tunatumia
fursa hii kumpongeza kwa kuonesha nia ya dhati ya kutekeleza agenda na maono
ambayo kama mashirika yanayotetea haki za wanawaketumekuwa tukiipigania kwa
muda mrefu sasa.

Tunapongeza
Serikali ya Awamu ya Sitakwa kazi wanayoifanya katika kusimamia utekelezaji wa
sera, na mipango ya maendeleo kwa manufaa ya taifa na watanzania. Hali
kadhalika yako mambo ambayo bado yanahitaji kuongezewa nguvu ili kuhakikisha
tunafikia lengo la kuwa na maendeleo endelevu yenye kujumuisha ustawi wa
makundi yote na kudumisha haki za msingi za binadamu ikiwemo usawa wa jinsia,
katika kufikia azma ya Serikali ya awamu hii ya kufikia uchumi shindani, viwanda
na maendeleo ya watu.

Tumeshuhudia
kuwepo kwa jitihada zenye lengo la kuboresha sekta za huduma kwa jamii, sekta
ambazo kwa kiwango kikubwa zinawagusa wanawake moja kwa moja. Jitihada hizo ni
pamoja na kuboresha miundo mbinu ya huduma za afya kama vile ujenzi wa
hospitali 99, hospitali 10za rufaa za mkoa, zahanati 1,198, ujenzi wa jengo la mama
na mtoto katika hospitali ya Mwananyamalana kufikia asilimia 51 ya kukamilika
kwa ujenzi wa jengo la kina mama na mtoto. katika mkoa wa Simiyu. Hatua hizi
zimechangia kwa kiasi fulani kupunguza vifo vya kina mama na watoto. Pamoja na
juhudi hizo bado kuna changamoto katika upatikanaji wa huduma za uzazi salama
bila gharama kubwa au tozo, hususani kwa wanaohitaji upasuaji.Tunaamini kuwa
hawa wanawake wanaoleta nguvu kazi ya taifa hawatakiwi kulipia huduma hiyo
kabisa kwani ili taifa liendelee linahitaji watu na wanaoleta watu duniani ni
wanawake; wanahitaji kuenziwa kwa kazi hiyo nzito.  Kwa upande mwingine, bado kuna upungufu wa
vituo vya afya na zahanati kwenye baadhi ya maeneo ya vijijini na mijini, jambo
ambalo linasababisha changamoto kubwa sana kwa wanawake hasa wale wajawazito na
waliofikia hatua ya kujifungua; bajeti pia haijaanisha kwa kiwango gani
imejipanga katika kupunguza upungufu wa watumishi wa afya; baadhi ya vituo vya
afya hasa vijijini havina huduma za maji na umeme.

Kwa
upande wa upatikanaji wa maji, Serikali imefanikiwa kwa kiwango fulani kumtua
ndoo mama vijini na mijini kwa asilimia 72.3 na 85 kufikia kukamilika kwa
miradi 1845 ya maji vijijini na mijini.  Pamoja
na miradi hii kukamilika lakini bado tatizo la maji ni changamoto maeneo mengi
hususani vijijni ambapo ndipo wananchi wengi wanaishi na pia kwenye taasisi za
umma kama vituo vya afya na taasisi za elimu. Tukumbuke kuwa maji ni huduma kwa
namna yoyote huduma ya maji isigeuke kuwa chanzo cha mapato au biashara. 

Kwa
upande wa elimu, Serikali imepanga kufanya mapitio ya Sera ya Elimu kuendana na
muktadha uliopo, tunatarajia ushiriki mpana wa wadau mbalimbali katika mchakato
huu muhimu. Pia,Serikaliimeendelea kuongeza fursa ya kila mtoto kwenda shule
kwa kugharamia elimu msingi bila ada.
Ikumbukwe kuwatangu elimu bila ada ianze sasa ni miaka 7, hivyo uhitaji
wa wanafunzi kuingia kidato cha kwanza utakuwa kubwa,ni matumaini yetu kuwa maandalizi
yamefanyika hasa katika kutenga rasilimali za kutosha kuhakikisha wanafunzi
wanaomaliza darasa la saba watapata fursa ya kuendelea na masomo ya sekondari
bila vikwazo.

Hata
hivyo, katika kumkomboa mtoto wa kike shuleni, bajeti imeendelea kuwa kimya
katika upatikanaji wa sodo (pedi/ taulo za kike) na miundo mbinu ya hedhi
salama kwa wanafunzi wa kike, walio kwenye mfumo wa elimu ya msingi na
sekondari. Bajeti haijataja mafungu au kutoa maelekezo yoyote kwa Halmashauri
za Wilaya, au mamlaka za elimu kuyazingatia mahitaji haya katika mafungu ya
fedha wanayopata. Kuna umuhimu wa serikali kutoa maelekezo ya kuwezesha
upatikanaji wa bajeti hii ili kuwasaidia wanawake na watoto wa kike kuondokana
na fedheha na changamoto za kiafya wanazokutana nazo wakiwa katika hedhi kwa
kukosa vifaa safi na salama vya kujisitiri wakiwa katika hedhi. Tunaendelea
kutoa wito kwa Serikali yetu ya Awamu ya Sitainayojali usawa wa jinsia kuondoa
tozo ya VAT kwenye pedi ambayo ilirudishwa mwaka 2019. Kama kodi ya
VATimeondolewa kwa bidhaa nyingine ni muhimu kuangalia hili suala kwa jicho
makini zaidi kusaidia wanawake na wasichana.

Katika
sekta ya kilimo, sekta ambayo inawaajiri wanawake kwa zaidi ya asilimia
57.  Serikali ya Awamu ya Sitaimetoa
kipaumbelekatika kuimarisha sekta ya kilimo kutoa mali ghafi kwa ajili ya
viwanda. Tunatarajia juhudi hizi zitasaidia ushiriki wa wakulima wadogo wadogo
ambao wengi wao ni wanawake ili waweze kufaidika na juhudi hizi. Hata hivyo,
bado bajeti haija chambua kwa umakini changamoto za ufikiaji wa maeneo ya
kilimo kwa vijana na wanawake, na kuhusu changamoto za ufikiaji wa masoko ya
bidhaa mbalimbali kwa wakulima wanawake na vijana. Aidha, Bajeti Kuu ya
Serikali pia haikuelekeza kwa ufasaha jinsi makundi ya wanajamii wanawake na
vijana wanavyostahili kuelekezewa mitaji na mikopo ya kilimo, au kuelekeza
kiwango fasaha mikopo na mitaji kwa makundi hayo.Tumefarijika kuwa gharama za
kulipia umiliki wa ardhi na kurasimisha ardhi zimepungua tunaipongeza serikali
kwa hili.

Kwa
upande wa uziduaji, bajeti ya Serikali Kuu na ile ya kwenye sekta ya uziduaji,
haijaainisha kwa ufasaha jinsi gani wanawake na vijana walio kwenye sekta ya
uziduaji wanamilikishwa na kulindwa kisheria katika maeneo yao ya uchimbaji, na
kupatiwa mitaji, mikopo, maarifa, na teknolojia chanya za kuboresha harakati
zao za kujichumia mapato kupitia sekta hii.

 

Kukabiliana
na mapungufu tuliyoainisha, tunapendeleza yafuatayo: 

 

Sekta
ya Elimu

Tunapendekeza
Serikali, kupita sekta ya elimu, VETA na SIDO kuhakikisha kwamba mafunzo ya
stadi mbalimbali za ufundi na sayansi yanaongeza udahili wa wasichana na vijana
wa makundi ya pembezoni ili kunufaika na ajira zenye tija. Pia, Serikali itoe maelekezo
kwa  Halmashauri za Wilaya kutenga
asilimia ya fedha za “capitation grant”
kuhudumia mahitaji ya hedhi salama kwa wanafunzi wa elimu ya msingi.

 

Sekta
ya Afya

Tunapendekeza,serikali
itenge bajeti yenye kulenga na kuhamasisha utoaji wa Bima za Afya kwa gharama
sawa na bure kwa wajane wenye uhitaji, wazee na wanawake na kaya masikini
nchini.  Pia, tunakumbusha serikali
kutimiza makubaliano ya Abuja, ambayo nchi imeridhia, ya kutenga asilimia 15 ya
bajeti kuu kwa jili ya bajeti ya afya. Tunatoa wito kwa Serikali na wadau
wengine kuongeza uwekezaji katika kutoa elimu ya umuhimu na namna ya kuzuia magonjwa
ili kupunguza gaharama za matibabu ya magonjwa yanayozuilika. Ujenzi wa uchumi
shindani wa viwanda na maendeleo ya watu unahitaji nguvu kazi ya afya bora.

 

Sekta
ya Maji

Tunapendekeza
Serikali kuelekeza sekta ya maji kutanua na kujazilisha (densification) mtandao wa huduma ya maji safi na salama, kwa kuweka
mikakati ya kupata fedha zitakazowezesha suala hilo. Pia, Serikali kuelekeza
sekta ya maji kuondoa tozo za maji kwa taasisi za umma kama shule na vituo vya
huduma za afya. Pia, Wizara ya maji kutoa maelekezo kwa idara za maji za mikoa kuwezesha
upatikanaji wa maji kwa wajane, wazee, kwa tozo za viwango vya chini kabisa, au
hata bila tozo yoyote. Vituo vya kulelea Watoto wenye chanagamoto na vituo vya
wazee vipewe maji bila gharama yoyote.

 

Sekta
ya Kilimo

Kufanikisha
ushiriki wa wanawake na vijana katika uchumi shindanishi, tunapendekeza  sekta ya kilimo itenge rasilimali za kutosha
kuwalenga wanawake na vijana katika ufikiaji wa mikopo ya masharti au riba
nafuu, upatikanaji wa teknolojia sahihi za uzalishaji na uhifadhi, na  ufikiaji rahisi wa masoko wezeshi, ufikiaji
sahihi wa taarifa za tafiti za mbegu bora na mifumo ya kilimo cha umwagiliaji,
upokeaji wa taarifa za tafiti za Taasisi za Kilimo, na kuwa wateja wakuu wa
Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB). Pia, Serikali izielekeze Halmashauri za
Wilaya kwa makusudi, kujenga masoko mapya kwenye maeneo yenye mvuto mkubwa kwa
bidhaa za wajasiriamali wanawake na vijana. Pia, tunakumbusha serikali kutimiza
makubaliano ya Malabo, ambayo nchi imeridhia, kutenga asilimia 10 ya bajeti kuu
kwa ajili ya bajeti ya kilimo. 

 

Sekta
ya Uziduaji

Tunapendekeza
sekta ya uziduaji ielekeze jitihada kubwa zaidi kuhakikisha vijana na wanawake
waliyo kwenye shughuli za uziduaji wanamilikishwa maeneo yao, wanapatiwa mafunzo
na teknolojia za uchimbaji wa kisasa, wanapewa taarifa za kitaalam kuhusu
upatikanaji wa madini, wanajengewa mbinu mpya za uchimbaji na uziduaji, na
kuhakikishiwa ufikiaji wa masoko na bei wezeshi kwa bidhaa zao za madini.

 

Kwa
ujumla tunapendekeza,

 

·       Bajeti
ya Serikali itoe matamko na maelekezo kwa watumishi wa Serikali kusimamia
utoaji wa asilimia 30 ya kandarasi za umma, na ajira wapewe wanawake, vijana na
watu wenye ulemavu kama sera na kanuni zinavyoelekeza.

·       Aidha
mifumo ya kidijitali iwe rafiki zaidi kwa wanawake na vijana wa pembezoni
katika kupasha na kupokea taarifa za kibiashara na masoko.

·       Bajeti
ya Serikali Kuu ielekeze sekta ya Viwanda na Biashara, na pia TAMISEMI,
kuongeza ufikiaji wa huduma za masoko kwa bidhaa zinazozalishwa na wanawake na
vijana wa pembezoni ili waweze kunufaika na uchumi shindani, na Maendeleo ya
viwanda.

·       Serikali
iongeze nguvu katika kubuni vyanzo vya mapato ambavyo havimuumizi au
kumuongezea mzigo mwananchi wa kawaida hususani wanawake. Kuongeza makato
kwenye mafuta kutamuongezea moja kwa moja mzigo mwananchi wa kawaida kwa
ongezeko hili kuna uwezekano mkubwa wa bidhaa na huduma mbambali kupanda
gharama.

 

Imetolewa
na,

Lilian
Liundi,

Mkurugenzi
wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)

Kwa
niaba ya wadau walioshiriki mjadala wa bajeti ya Taifa, 2021/22.