Home Michezo ITALIA YAANZA VYEMA EURO 2020, YAICHAPA 3-0 UTURUKI

ITALIA YAANZA VYEMA EURO 2020, YAICHAPA 3-0 UTURUKI

0

ITALIA imeanza vyema Fainali za Euro 2020 baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Uturuki usiku wa Ijumaa Uwanja wa Olimpico Jijini Rome.
Mabao ya Italia katika mchezo huo wa Kundi A yamefungwa na Merih Demiral aliyejifunga dakika ya 53, Ciro Immobile dakika ya 66 na  Lorenzo Insigne dakika ya 79 na kwa ushindi huo kikosi cha Roberto Mancini kinaanzia kileleni baada ya mechi hiyo ya ufunguzi leo.
Euro 2020 inaendelea leo kwa mechi tatu Wales na Uswisi Kundi A Saa 10:00 jioni na za Kundi B Denmark na Finland Saa 1:00 usiku na Ubelgiji na Urusi Saa 4:00 usiku.