Naibu Waziri wa Uwekezaji Mhe. William Ole Nasha akizungumza na wawekezaji ambao wana nia ya kuanzisha kiwanda cha kuunganisha Magari hapa nchini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya watoa huduma katika sekta ya Mafuta na Gesi nchini (ATOGS) Bw.Abdullsamad Abdulirahim akizungumza katika kikao cha wawekezaji na Naibu Waziri wa Uwekezaji Mhe.William Ole Nasha uliofanyika leo katika kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Jijini Dar es Salaam.
********************************
NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM
Uongozi wa Umoja wa watengenezaji wa magari Yaani Afrika automotive manufacturer wamefika nchini Tanzania na kufanya mazungumzo ya awali na Naibu Waziri wa Uwekezaji Mhe. William Ole Nasha juu ya nia yao ya kuanzisha kiwanda cha kuunganisha Magari hapa nchini.
Akizungumza jijini Dar es salama katika Ofisi za Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC), Mhe. Ole Nasha amesema kuwa ujumbe huo umefika kwa ajili ya kupata baraka za Serikali ili waweze kuanzisha kiwanda hicho nchini.
“Utengenezaji wa viwanda vya magari nchini utasaidia kupunguza gharana za uagizaji wa magari kutoka nje ya Nchi hatua ambayo itaongeza upataikanaji wa mapato yatakayotokana na kodi”. Amesema Mhe.Ole Nasha.
Kwa upande wake mwenyekiti wa jumuiya ya watoa huduma katika sekta ya mafuta na gesi nchni ATOGS Bw.Abdullsamad Abdulirahim akiwa ameongozana na ujumbe huo amesema kuanzishwa kwa kiwanda hicho kutatoa fursa za ajira lakini pia kupunguza gharama za ununuaji wa magari.
Miongoni mwa wageni hao ni Rais wa umoja watengenezaji wa magari yote Afrika.