********************************
Jamii ya watu wanaoishi na ugonjwa wa selimundu nchini, (Sicko cell), wameiomba wizara ya afya kuweka mpango kazi ambao utawezesha ugonjwa huo kuboresha upatikanaji wa upimaji wa ugonjwa huo ili kufanikisha kupunguza watoto wengi kuzaliwa na tatizo hilo.
Ombi hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya wagonjwa wa selimundu Tanzania, Arafa Said, katika hafla ya kuelekea maadhimisho ya siku ya ugonjwa selimundu Duniani inayoazimishwa kila june 19 ya kila mwaka.
Endapo kama upimaji utaanzia ngazi ya chini basi itarahisisha watu wengi kufahamu hali zao za afya na kushauriwa vitu vya kuzingatia kabla ya kuolewa au kuoa na hatimaye kupata mototo”. Amesema Bi.Arafa.
Aidha maombi mengine yaliyoombwa ni pamoja ushirikiano kutoka serikalini katika kuweka sera na mipango kazi ambayo itaboresha utolewaji wa huduma za afya, kuweka mpango kazi ambao utawezesha selimundu kujumuishwa katika mpango wa Taifa wa bima ya afya,kufikisha huduma kwa mwana jamii ambae anaishi katika vijiji vya ndani ndani.
Pia WameiombaWizara pamoja na washirika kusaidia ufadhili na kuwezesha upatikanaji wa huduma za kliniki za selimundu katika mikoa ile iliyoathiriwa pamoja na kupanua upatikanaji wa huduma nje ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Dkt Astellia Mpoto kutoka Wizara ya afya idara ya Tiba, kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukizwa na msimamizi wa ugonjwa selimundu kitaifa, amewataka wagonjwa wa sicko seli kuwa na bima ya afya ili kupunguza gharama za matibabu huku akiwataka wanaotarajiwa kuingia kwenye mahusiano kupima kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Katika hafla hiyo baadhi ya wasanii na watu maarufu wamejitokeza kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii ili kufahamu ugonjwa huo
Dkt, Deogratias Soka ni Mkurugenzi mtendaji wa asasi zinazojihusisha na mambo ya ugonjwa sicko cell amewasihi wazazi kutokulaumiana pindi watakapozaa motto mwenye maradhi hayo.
Maadhimisho ya siku ya ugonjwa selimundu (SICKOCELL), Duniani kitaifa yanatarajiwa kuadhimishwa jijini Mwanza june 19.