Home Mchanganyiko WAZIRI UMMY ATAKA MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI NA WACHUMI SEKRETARIETI ZA MIKOA KUCHAMBUA...

WAZIRI UMMY ATAKA MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI NA WACHUMI SEKRETARIETI ZA MIKOA KUCHAMBUA NA KUPITIA MIPANGO YA BAJETI YA HALMASHAURI

0

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Ummy Mwalimu ,akizungumza na Makatibu Tawala Wasaidizi na wachumi wa Sehemu za Mipango na Uratibu katika Sekretarieti za Mikoa nchini kikao kilichofanyika leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Ummy Mwalimu ,akiwasisitiza jambo Makatibu Tawala Wasaidizi na wachumi wa Sehemu za Mipango na Uratibu katika Sekretarieti za Mikoa nchini wakati wa kikao kilichofanyika leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

……………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

SEREIKALI imewaagiza Makatibu Tawala Wasaidizi na wachumi wa Sehemu za Mipango na Uratibu katika Sekretarieti za Mikoa nchini kuhakikisha wanapitia, kuchambua na kutoa ushauri kwenye mipango ya bajeti za maendeleo za Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hayo yamesemwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.Ummy Mwalimu wakati akizungumza na viongozi hao amesema kuwa jukumu lao ni kuhakikisha wanapitia na kuchambua kwa umakini mkubwa Mipango ya bajeti za maendeleo zinazoletolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuangalia vipaombele vya Serikali katika kutatua kero za wananchi.

“Kazi yenu si ya kukusanya taarifa za bajeti zinazoandaliwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa pekee, bali mnawajibu wa kuzichachambua kwa weledi kwa kungalia vipaombele vya Serikali vya kutatua changamoto za wananchi katika sekta ya elimu, afya, barabara na mikopo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu,” amesema Mhe.Ummy

Amesema  kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha fedha zinazokusanywa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo inatatua changamoto za wananchi.

Aidha amewaagiza kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatenga fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ambapo Halmashauri zinazokusanya zaidi ya shilingi Bilioni 50 zinatakiwa kutenga asilimia 60 ya fedha hizo kwa miradi ya Maendeleo wakati Halmashauri zinazokusanya chini ya bilioni 50 zinatakiwa kutenga asilimia 40.

Amesema kuwa serikali inataka kuona Halmashauri zote nchini zinatenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa vituo vya afya, zahanati,ununuzi wa vitendanishi na dawa, ujenzi wa madarasa, ununuzi wa madawati, ujenzi wa mabweni, hivyo ni jukumu la makatibu tawala hao kuhakikisha mipango hiyo inaingizwa kwenye Mipango ya bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Unapitishaje Bajeti ya Halmashauri wakati haina bajeti ya ujenzi wa madarasa, ununuzi wa dawa na vitendanishi, ujenzi wa shule, mabweni na madawati, hii haikubaliki kasimamieni na kuhakikisha bajeti hizo zinakidhi mahitaji ya wananchi.” amesema Ummy.

Waziry Ummy amewasisitiza Makatibu Tawala Wasaidizi wote nchini kuhakikisha wanasimamia utengaji wa fedha za kuwawezesha wananchi kiuchumi ikiwemo mikopo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili ikalete tija kwa jamii, pia amewataka kuhakikisha fedha hizo zinatolewa kwenye vikundi ambavyo vinaleta tija katika jamii ili kuongeza tija kwa maeneo husika na kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa kwa wakati.

Aidha Waziri Ummy awataka Makatibu Tawala wasaidizi na wachumi sehemu ya Mipango na Uratibu kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatenga bajeti kwa ajili ya uendelezaji wa miji na vijiji kwa kwa maendeleo hayatapatikana kama hatutawekeza katika uendelezaji miji na vijiji nchini