Home Mchanganyiko TANZANIA YASAINI MKATABA WA MKOPO WA ZAIDI YA BILIONI 361 KUGHARAMIA UMEME...

TANZANIA YASAINI MKATABA WA MKOPO WA ZAIDI YA BILIONI 361 KUGHARAMIA UMEME WA JUA

0

Katibu Mkuu Wizara ya fedha na Mipango Emmanuel Tutuba kulia na Mkurugenzi Mkazi wa shirika la maendeleo la Ufaransa Bi. Stephanie Essombe wakisainiana mkataba wa mkopo wa mashart nafuu  wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

Balozi wa Ufaransa hapa nchini Bw. Fredric Clavier, kulia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na mipango Emmanuel Tutuba katikati wakionyesha mikataba mara baada ya kusainiana kwa   mkataba wa mkopo wa mashart nafuu  wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya fedha na mipango Emmanuel Tutuba akizungumza mara baada ya hafla ya kusainiana mkataba wa mkopo wa mashart nafuu  wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi mkazi wa shirika la maendeleo la Ufaransa hapa nchini, Bi. Stephanie Essombe akizungumza mara baada ya hafla ya kusainiana mkataba wa mkopo wa masharti nafuu  wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,1021 jijini Dodoma.

Balozi wa Ufaransa hapa nchini Bw. Fredric Clavier akizungumza mara baada ya hafla ya kusainiana mkataba wa mkopo wa mashart nafuu wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa shirika la umeme hapa nchini TANESCO, Dkt Tito Mwinuka akizungumza mara baada ya hafla ya kusainiana mkataba wa mkopo wa mashart nafuu  wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya fedha na mipango, Emmanuel Tutuba wa pili kutoka kulia waliokaa akiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya hafla ya kusainiana mkataba wa mkopo wa mashart nafuu  wa shilingi bilioni 361.71 kwa ajili ya ujenzi wa mitambo ya uzalishaji wa umeme wa jua, mkataba uliosainiwa leo Juni 11,2021 jijini Dodoma.

…………………………………………………………………………

Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.

Tanzania na nchi ya Ufaransa kupitia mradi wa shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD), zimesaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wenye thamani ya Euro milioni 130 sawa na shilingi bilioni 361. 71 fedha za kitanzania kwa ajili ya mradi wa mitambo ya kuzalisha umeme wa jua, mradi unaotarajiwa kutekelezwa Wilaya ya Kishapu, Shinyanga.

Akizungumza mara baada ya kusainiwa kwa mkataba huo Katibu Mkuu Wizara ya fedha na mipango, Emmanuel Tutuba amesema mradi huo  ni wa mwaka mmoja ambao unatarajiwa kuanza marchi 2022 hadi 2023.

“Lengo la mradi huu ni kujenga mitambo ya kuzalisha umeme wa jua kiasi cha megawatt 150 katika Wilaya ya kishapu Mkoani Shinyanga, mradi huo unatarajiwa kuwa na awamu mbili ambapo kwa awamu ya kwanza tutaanza na megawatt 50” amesema Tutuba.

Katibu Tutuba amebainisha kuwa sehemu ya fedha hizo zitatumika kuboresha na kuimarisha grid ya taifa kuifanya kuwa ya kisasa kuweza kujumuisha umeme wa nishati jadidifu zenye muda maalumu na pia kupunguza upotevu wa umeme.

Ameongeza kuwa “Nafahamu pia kuwa AFD ilitoa msaada wa kufanya upembuzi yakinifu wa mradi huu, na kuwa kiasi cha Euro laki 7 kimetengwa na serikali ya ufaransa kama msaada wa kitaalamu katika mradi” amesema.

Amesema kupitia mradi huo ni kuongeza uhakika wa upatikanaji wa nishati ya umeme ili kuiwezesha TANESCO kutimiza malengo ya kuzalisha umeme kutoka katika vyanzo mbalimbali kwa kutumia nishati jadidifu.

“Mradi huu utapunguza utegemezi wa umeme wa nguvu za maji wakati wa jua hivyo kuwa na uwezo wa ziada wa uzalishaji ambao utatumika majira ya mahitaji makubwa ya umeme wakati wa ukame” amesema.

Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania ameishukuru Serikali ya Ufaransa kupitia mkurugenzi wa AFD kwani mkopo huo kwani utasaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika migodini na uhakika wa umeme katika grid ya taifa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa AFD, Bi. Stephanie Essombe amesema wataendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na wanafurahi kuwa sehemu ya mradi huo utakao weza kuleta maendeleo kwa watanzania.

Amesema mradi huo utakaoendeshwa kiteknolojia utaongeza utaongeza fulsa kwa watanzania katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuchochea uchumi shindani, kukuza uwekezaji na biashara na kuchochea maendeleo ya watu.

Amesema kwa mkataba uliosainiwa leo wa Euro milion130 utawezesha maendeleo kwa TANESCO na kufanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache zenye teknolojia hiyo barani Afrika.

Nae Balozi wa Ufaransa hapa nchini Bw. Fredric Clavier amesema Tanzania na Ufaransa wana uhusiano mzuri na wataendelea kushirikiana na Tanzania katika nyanja mbalimbali ya kiuchumi hapa nchini.

Akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Leonard Masanja, Mtendaji Mkuu wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO Dkt Tito Mwinuka amesema kukamilika kwa mradi huo utapunguza upotevu wa megawatt kwenye grid ya taifa na kuahidi kusimamia ipasavyo mradi huo na kuhakikisha unakamilika kwa wakati.