Home Mchanganyiko SPIKA AFUNGUA MAJADILIANO YA WABUNGE KUHUSU UCHUMI

SPIKA AFUNGUA MAJADILIANO YA WABUNGE KUHUSU UCHUMI

0

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai (Mb) akizungumza wakati akifungua majadiliano  ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma.  Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe Tulia Ackson, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti Mhe. Daniel Baran Sillo na Katibu wa Bunge Ndg. Nenelwa Mwihambi,

Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mada wakati wa majadiliano  ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. Mada zilizotolewa ni pamoja na umuhimu wa takwimu katika kukuza uchumi, mchango wa taasisi za sera katika maedeleo ya uchumi wa jamii, sera za Kibajeti na Uchumi Jumuishi.

Mtakwimu Mkuu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa mada umuhimu wa takwimu katika kukuza uchumi wa nchi wakati wa majadiliano  ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma. 

Kamishna wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango  Ndg. William Mhoja,  akitoa mada  kuhusu Sera za kibajeti wakati wa majadiliano  ya Wabunge kuhusu masuala ya Uchumi yaliyofanyika katika ukumbi wa Msekwa Bungeni Jijini Dodoma