Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiupongeza mkakati ulioandaliwa kwa lengo la kusaidia kuvitangaza vivutio vya utalii vya kusini mwa Tanzania
Baadhi ya wadau wa utalii waliohudhulia kwenye mkakati wa kuhakikisha wanavitangaza vivutio vya kitalii vya kusini mwa Tanzania
Picha ya pamoja ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga na wadau wa utalii kusini mwa Tanzania.
Normal
0
false
false
false
EN-US
X-NONE
X-NONE
MicrosoftInternetExplorer4
/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin:0in;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa mkoa wa Iringa amepongeza
mikakati ya bodi ya utalii (TTB) ya kutangaza vivutio vya kitalii vilivyopo
kusini mwa Tanzania ambavyo vitachochea kukuza uchumi wan chi na kuleta
maendeleo kwa ujumla.
Akizungumza kwenye kikao cha
mikakati ya kutangaza vivutio hivyo, Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga
alisemakuwa bodi ya utalii imejitahidi kwa kiasi kikubwa wametangaza vivutio
vya kusini mwa Tanzania kwa njia mbalimbali ikiwa ndani ya nchi hadi nje ya
nchi ambako wameongeza watalii kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa TTB kwa
ushirikiano na wadau wa utalii wanatakiwa kuendelea kuvitangaza vivutio hivyo
kwa kasi kubwa ili kukuza vipato vya wananchi na kukuza pato la taifa na
kuchangia maendeleo ya nchi kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati na
ile ambayo imebuniwa na watalaam.
Sendiga aliiomba bodi ya Utalii
(TTB) kuendelea kuongeza mikakati ya kuvitangaza vivutio vilivyopo kusini mwa Tanzania
kwa kuwa bado kuna vivutio vya kitalii vingi havijatangazwa kama inavyotakiwa
kama ambavyo vinatangazwa vivutio vingine.
Alisema kuwa mkoa wa Iringa ni
mmoja ya mkoa ambao unavivutio vingi na unafikika kwa kirahisi hivyo kuendelea
kuvitangaza vivutio hivyo vitachangia kuleta maendeleo ya mkoa wa Iringa kwa
kasi kubwa na kupokea watalii wengi.
Sendiga aliwaomba wadau wa maswala
ya utalii kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya barabara,huduma bora za hotel
kwa lengo la kuwavutia watalii wengi kuja mkoani Iringa kwa kuwa kunavivutio
vingi ambavyo kwa kiasi kikubwa kunasaidia kukuza pato la nchi.
Kwa upande wake kaimu meneja wa
mikutano na matukio kutoka bodi ya utalii Tanzani,Irene Mvile alisema kuwa
wadau wa utalii kwa kushirikiana na serikali kwa pamoja wanaweza kutekeleza
mkakati huo wa kukuza utalii wa kusini mwa Tanzania na kukuza pato la taifa kwa
ujumla kwa kuongeza idadi kubwa ya watalii kutembelea vivutio vilivyopo.
Alisema kuwa wadau wa kusini
ndio wanajua vivutio vilivyopo kusini mwa Tanzania na namna ya kuvitangaza
hivyo wadau wanapaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali ili kufanikisha
kuvitangaza vivutio vilivyopo.
Aliongeza kwa hivi sasa wapo na
wataalam wa kusaidia kuvitangaza vivutio vilivyopo kusini mwa Tanzania kwa
kuanza kutoa semina kwa wadau wa utalii wa
kusini mwa Tanzania ili wajue namna ya kuwavutia watalii na kuvitangaza vivutio
vilivyopo.