Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Rawan Dakik (wa nne kutoka kushoto) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kutangaza Mlima Kilimanjaro, katika hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro . Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza Rawan kama Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella(wa nne kutoka kulia) wazazi wa Rawan, Mbunge wa Arusha Mjini,
Mhe. Mrisho Gambo(wa tatu kutoka kulia),Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe.Jerry Muro (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TTB , Betrita Lyimo (kulia)
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi ua Rawan Dakik (katikati) ikiwa ni ishara ya kumkaribisha baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro akitokea bara la Asia alikopanda Mlima Everest.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiteta jambo na wazazi wa Rawan kabla ya hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza Rawan Dakik kama Balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro.
******************************
Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua Rawan Dakik kuwa balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kutambua jitihada zake za kutangaza Mlima Kilimanjaro, baada ya kupanda mlima huo kwa takriban mara tano na pia kuipeperusha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima mrefu zaidi duniani Everest uliopo bara la Asia.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Rawan Dakik yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro leo.