Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akifafanua jambo juu ya Mashirikiano kati ya Makumbusho ya Taifa Bar na Makumbusho na Mambo kale Zanzibar, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho na Mambo Kale Zanzibar Bw Salim Sululu
Mratibu wa mashirikiano kati ya Makumbusho ya Taifa na Makumbusho na Mambo ya Kale Zanzibar Bw Revocatus Bugumba akifafanua jambo kwenue kikao cha wataalam wa Makumbusho Bara na Zanzibar, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho na Mambo Kale Zanzibar Bw Salim Sululu.
Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga akizungumza na wataalam wa Makumbusho ya Taifa Bara na Makumbusho na Mambo Kale Zanzibar katika kikao cha Kuanzisha Mashirikiano.
Juu na chini ni wataalam wa Makumbusho ya Taifa Bara na Makumbusho na Mambo Kale Zanzibar wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho na Mambo Kale Zanzibar Bw Salim Sululu katika kikao cha Kuanzisha Mashirikiano
****************************
Na Sixmund J. Begashe
Kumekuwa na mashirikiano mengi kati ya Tanzania Bara na Tanzania Visiwani lakini si katika sekta za Makumbusho na Mambo kale hivyo Taasisi ya Makumbusho ya Taifa Tanzania Bara na ile ya Makumbsho na Mambo Kale ya Zanzibar zimeamua kuanzisha mashirikiano katika nyanja mbali mbali ili kuhifadhi na kuendeleza urithi wa kiutamaduni na Mali Kale nchini.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noel Lwoga katika kikao cha mashirikiono kati ya Makumbusho ya Taifa Tanzania Bara na Makumbusho na Mambo Kale Zanzibar kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam.
Dkt Lwoga ameleza kuwa Taasisi yake imeona upo umuhimu wa Taasisi hizi mbili kushirikiano hasa katika nyanja ya kubadilishana utaalamu, ushirikiano katika matukio ya Kitaifa yanayohusu Makumbusho na Mambo ya Kale, kutangaza shughuli na vivutio vya Taasisi zote mbili pamoja na katika miradi inayohusiana na Makumbusho na Mambo ya Kale.
Akizungumzia mashirikiano hayo, Mkurugenzi wa Mkumbusho na Mambo Kale Zanzibar Bw SALIM SULULU amesema, Tanzania Bara na Visiwani zina mahusiano makubwa ya ki ikolojia na kihistoria ambavyo taarifa zake zimehifadhiwa kwenye Makumbusho zote zilizopo Bara na Visiwani hivyo ni vyema sasa Taasisi hizi zikashirikiana ili kuboresha huduma za uhifadhi wa urithi wa asili na mambo ya kale.
”Niipongeze Makumbusho ya Taifa Bara chini ya Dkt Lwoga, wenzetu huku wameendelea sena katika suala zima la utafiti, ukusanyaji na uhifadhi wa matokeo ya tafiti ya mambo ya Kimakumbusho na Mali Kale, sisi Zanzibar tupo vizuri zaidi katika kutembelewa na wageni, kwenye vivutio vya Makumbusho na Mambo kale hivyo ni wakati muafaka sasa tukashirikiana ili tupate kujifunza kutoka huku na wao wajifunze kutoka kwetu” Aliongeza Bw Sululu.
Naye Muhifadhi Mwandamizi kutoka Makumbusho Zanzibar Bi Farida Senga amefurahishwa kwa kukutana na wataalam wa Makumbusho ya Taifa Bara na kusema kuwa huu ni mwanga mpya katika maendeleo ya uhifadhi na uendelezwaji wa Makumbusho na Mambo Kale kwa pande zote mbili.
”Kuna faida kubwa sana kwa sisi tukishirikiana, maana uzoefu nilionao nitawashirikisha sasa wenzangu wa hapa Bara, na wao watatushirikisha uzoefu wao, nilitamani sana kuona haya mashirikiano tangu huko nyumba lakini sasa imekuwa, ninatamani kuwa taratibu zitakamilika haraka ili mambo haya yaanze kufanya kazi” alisema Bi Senga.
Akizungumzia kuhusu mashirikiano hayo, Muhifadhi Mkuu wa Mambo ya Kale wa Makumbusho ya Taifa Bw Revocatus Bugumba ambaye pia ni mratibu wa mashirikiano ya Taaisisi hizo ameleza kuwa pande zote mbili zimeazimia kuunda kamati maalumu itakayo ratibu mchakato mzima wa zoezi hilo ili mashirikiano hayo yaanze mapema.