*************************
Na Silvia Mchuruza ,
Bukoba,Kagera.
Benki ya CRDB kupitia tawi lake la Bukoba imefanya kongamano la kuwainua wanawake kiuchumu katika Manispaa, lililoenda sambamba na ufunguzi wa akaunti ya malkia kwa akina mama.
Mbunge wa jimbo la Bukoba Mjini adv. Stephen Byabato amechangia kiasi cha fedha kwa ajiri ya kuwezesha akaunti za akina Mama wote walioshiriki kongamano hilo.
Akizindua kongamano hilo lililofanyika katika bwalo la Bukoba Sekondari mjini humo, mkuu wa Wilaya ya Bukoba Bw.Deodatus Kinawiro aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge ameishukuru CRDB kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali katika adhima yake ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.
DC Kinawiro amesema taasisi za kifedha kama CRDB imekuwa chachu kwa akina mama wengi na vijana kujikwamua kiuchumi kwa kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na taasisi hizo.
Meneja wa benki hiyo kanda ya ziwa, amesema kwasasa CRDB pamoja na kuwa na bidhaa ya akaunti ya malkia ambayo imewezesha akina mama wengi kujiunga pia imekuja na huduma nyingine ambayo akina mama wanaweza kuitumia kukua kiuchumi.
“Toka 2009 tuliwaanzishia akina mama akaunti ya Malkia ambayo haina makato lengo lake lilikuwa ni kuwawezesha akina mama kuhifadhi fedha zao sehemu salama na kuachana na kuficha fedha kwenye vibubu au ardhini na sasa tumekuja na mkopo kwa akina mama kwa kutumia akaunti hiyo ya malkia ambapo mteja anaweza kutumia asilimia themanini ya akiba yake kukopa na hii itawasaidia kuongeza mitaji na kukuza biashara zao.” Amesema meneja kanda ya ziwa
Katibu wa mbuge wa jimbo la Bukoba mjini Eng. Pasaka Bakari Kilaka akikabidhi fedha hiyo, amesema mbunge na Naibu Waziri wa Nishati amelichukulia kongamano hilo kwa uzito wa kipekee na kusema kuwa ataongeza kiasi cha fedha kwa kila mwanamke atakayefungua akaunti ya malkia ili fedha hiyo ikawe chachu kwa mama hao