Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wanachama wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO) kilichofanyika leo June 10,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wamilkiki na Mameneja wa Shule na Vyuo visivyokuwa vya Kiserikali Nchini (TAMONGSCO), Alfred Luvanda, akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Umoja huo uliofanyika leo June 10,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene amesema Serikali itazichukulia hatua kali Jumuiya zote zilizopo chini ya Wizara yake ambazo zitakiuka sheria na taratibu katika kujiendesha.
Akizungumza leo June 10,2021 Jijini Dodoma na Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo binafsi nchini (TAMONGSCO),Waziri Simbachawene amesema wale ambao wamekuwa na utaratibu wa kuleta vurugu na kuzivuruga Jumuiya,Wizara yake itachukua hatua kali ambapo amedai ikiwezekana hata pingu zitatumika.
“Ikipidi pingu itatembea haiwezekani mtu akawa anavunja sheria halafu anangaliwa tu na Mimi nitatuma Vyombo vya kufanya uchunguzi na tutachukua hatua kali kwa sababu wamekiuka Sheria za Nchi.
“Songeni mbele atakaeleta shida mimi ndio nitakaeshughulika nae na salamu hizi ziwafikie jumuiya hizi zinaundwa kwa mujibu wa sheria za Nchi haiwezekani watu
wakawa wanafanya fanya masihara tutachukua hatua kali kwa wale ambao wanavuruga vuruga.
Amesema Jumuiya hizo zilizoanzishwa na zinazofanya mambo mazuri katika Nchi haiwezekani mtu mmoja akaleta ugumu hivyo Wizara itachukua hatua za kisheria na mwenye kuchukua hatua hizo ni yeye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki na Mameneja wa Shule na Vyuo Binafsi nchini ( TAMONGSCO),Alfred Luvanda amesema wanamshukuru Waziri kwa kusimamia zoezi la uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa Shirikisho hilo halali ambapo amedai sasa watakuwa na uhuru wa kufanya Mambo yao pamoja na kuzungumza na Serikali namna gani wanaenda katika ubia wa uendeshaji pamoja shule nchini.
Naye,Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo,Youstor Mtungi amesema,wanakabiliwa na Changamoto ya baadhi ya wenye shule kuchukuliwa kama wafanyabiashara kwa kutozwa kodi nyingi wakati wao wapo kwenye lengo la kutoa huduma ya kumsaidia mtoto yoyote wa Mtanzania
Amesema lengo lao ni kukaa na Serikali ili waone jinsi gani wanamsaidia mtoto wa Kitanzania ambapo amedai wanatambua lengo la kutoa elimu ni wajibu wa Serikali kwa kila mtoto wa Kitanzania lakini wao watasaidiana ili kuhakikisha elimu inayotolewa inakuwa na ubora.
Hata hivyo,aliwakaribisha wamili na shule binafsi kujiunga na Shirikisho hilo ili waweze kuzitatua Changamoto kwa pamoja.