Mkutano wa Makatibu Wakuu
wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki umefanyika jijini Arusha tarehe 10 Juni 2021.
Mkutano huo ambao ulitanguliwa
na Mkutano kwa Ngazi ya Wataalam uliofanyika tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 jijini
hapa, pamoja na mambo mengine umekamilisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa
kwenye Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta
linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika tarehe
11 Juni 2021.
Miongoni mwa agenda zitakazowasilishwa
kwa Mawaziri ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye
vikao vilivyopita; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa
Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu ombi
la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kujiunga na EAC; Taarifa kuhusu hatua
iliyofikiwa ya utatu wa Jumuiya za EAC-COMESA-SADC katika Eneo Huru la Biashara
Barani Afrika na Taarifa ya Uchangiaji wa Bajeti ya EAC kutoka Nchi Wanachama.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano
wa Ngazi ya Makatibu Wakuu umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Prof. Sifuni Mchome. Viongozi wengine walioshiriki Mkutano huo ni
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Dkt.
Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na
Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na
Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Stephen Mbundi.
Sehemu ya ujumbe wa Kenya ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu |
Sehemu ya ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano wa MakatibuWakuu |
Sehemu ya ujumbe wa Rwanda ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu |
Sehemu ya ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu |
Ujumbe wa Sudan Kusini |
Prof. Mchome akiwa amesaini Ripoti ya Makatibu Wakuu itakayowasilishwa kwa Mawaziri |
Mjumbe kutoka Sudan Kusini naye akisaini Ripoti hiyo |
Mjumbe wa Uganda akisaini ripoti hiyo |
Mjumbe wa Kenya akisaini ripoti hiyo |
Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu |
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu |