Home Michezo GEITA YAICHAPA LINDI 3-1

GEITA YAICHAPA LINDI 3-1

0

********************************

Na Mathew Kwembe, Mtwara

Mabingwa wa UMITASHUMTA mwaka 2019, Geita wanaendelea vema na kampeni yao ya kulitetea kombe hilo baada ya kuisambaratisha timu ya soka ya mkoa wa Lindi kwa magoli 3-1.

Nyota wa mchezo huo ni mshambualiaji hatari wa timu hiyo Said Marko ambapo katika mchezo wa leo alifunga magoli mawili.

Goli lingine la timu ya Geita lilifungwa na winga machachari wa timu hiyo Enock Peter ambaye mara kwa mara aliisumbua ngome ya Lindi.

Goli la kufutia machozi kwa upande wa timu ya mkoa wa Lindi lilifungwa na mchezaji wa kutumainiwa wa timu hiyo Hassan Rove.

Huu ni mchezo wa pili kwa Geita ambapo tayari imekwishazifunga Morogoro magoli 4-0 na Lindi 3-1.

Geita inakabiliwa na michezo mingine katika kundi hilo ikiwemo Mbeya, Njombe, Mtwara na Kigoma.

Matokeo mengine ya michuano hiyo ya UMITASHUMTA inaonyesha kuwa Mara na Simiyu zimetoka sare kwa kufungana magoli 3-3, Iringa imeifunga Singida 3-1, Tanga imeichapa Dodoma 2-0, Ruvuma imefungwa na Kagera 0-1 na Mwanza imeishindilia magoli Arusha 7-0 huku Manyara ikikubali kipigo kutoka kwa Rukwa kwa magoli 1-2.

Matokeo mengine ya soka wavulana yanaonyesha Shinyanga imetoka sare na Kilimanjaro 2-2, Katavi ikiifunga Tabora 3-0 na Morogoro ikipata kipigo kingine kutoka kwa Mtwara 0-4.

Matokeo ya mchezo wa Netiboli yanaonyesha kuwa Mwanza imeifunga Mara kwa magoli 40-25, Morogoro imeilaza Tabora 24-22, Njombe dhidi Pwani matokeo ni 10-24, huku Kagera ikiifunga Singida 32-10, Dodoma imekubali kipigo kutoka kwa timu ya Netiboli Kigoma 12-19 na Mbeya imeibugiza Rukwa magoli 31-2

Kwa upande wa mpira wa mikono wavulana hadi mwamuzi anapuliza filimbi ya mwisho Kagera 5 Tabora 15, Manyara 11 Simiyu 8, Manyara 11 Simiyu 8, Mbeya 10 Geita 8

Matokeo ya mchezo wa mpira wa mikono kwa wasichana yanaonyesha Lindi 6 Simiyu 7,Ruvuma 4 Katavi 8, Dar es salaam 4 Songwe 9, Geita 10 Singida 13 na Iringa 7 Njombe 7.

Matokeo ya mechi za makundi mpira wa wavu wasichana yanaonyesha kuwa  Geita imeifunga  Pwani seti 3-0, na Mtwara imeifunga Lindi seti 3-0.

Mpira wa wavu kwa wavulana matokeo Kilimanjaro imeifunga Rukwa seti 3-0, Simiyu imeifunga Morogoro seti 3-2 na Iringa imefunga Pwani seti 3-0.

Kwa upande wa matokeo  ya mpira wa goli wavulana Lindi imeifunga Katavi magoli 16-10, Arusha imeichapa Tanga 15-9 na Manyara imeifunga Njombe magoli 13-8.

Matokeo ya mpira wa goli wasichana Tanga imeifunga Mwanza magoli 19-4, Morogoro imeilaza Rukwa 17-5 na Arusha imetoka sare na Kilimanjaro kwa kufungana magoli 4-4.

Michuano hiyo ya UMITASHUMTA ambayo inaendelea katika viwanja vya Chuo cha Ualimu Mtwara na Shule ya ufundi imekuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Mtwara na maeneo ya jirani.