…………………………………………………………………………….
Na Mathew Kwembe, Mtwara
Timu za Netiboli za mikoa ya Mwanza na Dar es salaam zimeibuka kuwa tishio kwenye michuano inayoendelea ya UMITASHUMTA katika viwanja vya shule ya Ufundi Mtwara na Chuo cha Ualimu baada ya kuzifunga bila huruma timu za mikoa ya Ruvuma na Singida.
Katika matokeo hayo, Dar es salaam iliibugiza Ruvuma kwa magoli 45-05 huku Mwanza ikiigalagaza Singida magoli 58-09.
Matokeo mengine ya Netiboli yanaonyesha kuwa Mbeya iiifunga Shinyanga magoli 15-09, Dodoma ikaichapa Songwe magoli 09-04, Manyara ikachapwa na Geita magoli 07-27 na Arusha ilifungwa na Kigoma magoli 11-18
Matokeo ya mpira wa wavu kwa michezo iliyochezwa leo jioni kwa timu ya wavulana inaonyesha Iringa ilifungwa na Mwanza seti 3-0, Pwani dhidi Tabora seti 3-1, Katavi dhidi Ruvuma seti 3-0, Dodoma dhidi Manyara seti 3-0, Lindi ikaifunga Arusha seti 3-0 na Geita ikaifunga Kagera seti 3-0.
Matokeo ya mpira wa wavu kwa wasichana yanaonyesha Kilimanjaro imeichapa Simiyu seti 3-0, Dodoma dhidi ya Songwe seti 3-2, Manyara dhidi ya Singida seti 3-0, Katavi dhidi ya Geita seti 3-0, Mwanza ikaifunga Tabora seti 3-0, Mara ikaichapa Rukwa seti 3-0.
Kwa upande wa mpira wa mikono matokeo ya michezo iliyochezwa leo inaonyesha kuwa timu ya mkoa wa Dar es salaam wavulana ikaifunga Pwani magoli 16-15, Geita imeichapa Lindi magoli 21-13, Dodoma imeifunga Shinyanga magoli 10-9 na Rukwa imeifunga Katavi magoli 12-7.
Kwa upande wa mpira wa mikono wasichana Tanga imeifunga Simiyu magoli 15-10, Songwe dhidi ya Tabora magoli 9-0, na Kigoma ikaifunga Pwani magoli 10-5.
Matokeo ya mpira wa goli wavulana yanaonyesha Geita ikaifunga Manyara magoli 15-11, Dodoma ikaibamiza Arusha magoli 21-7, Singida ikaifunga Iringa magoli 24-15, Morogoro ikaichalaza Ruvuma magoli 19-6, Rukwa ikaichapa Mwanza magoli 11-9, Mbeya ikaifunga Dar es salaam magoli 16-14 na Tabora ikaichapa Singida magoli 15-5.
Kwa upande wa mpira wa goli wasichana Tabora ikaifunga Lindi magoli 13-1, Njombe imeifunga Mwanza magoli 23-2, Kigoma ikaichapa Mara magoli 5-3, Ruvuma imeifunga Kilimanjaro magoli 10-9 na Tabora ikaichabanga Singida magolio 15-5.
Katika mchezo wa soka, timu ya wavulana kutoka mkoa wa Shinyanga ikaifunga Mara magoli 4-0, Mwanza dhidi ya Kilimanjaro matokeo ni 1-1, na Songwe ikaichabanga Arusha magoli 7-4.
Matokeo ya mchezo wa soka kwa wasichana Lindi ikaifunga Katavi magoli 2-0, Geita imeichapa Kilimanjaro magoli 2-0, na Mwanza imeifunga Singida magoli 4-2.
Michuano hiyo ambayo bado ipo katika hatua ya makundi itaendelea kuchezwa kesho katika viwanja mbalimbali vya chuo cha ualimu Mtwara na Shule ya Ufundi.