MENEJA
wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nelson Mlali akizungumza
na waandishi wa habari mjini Tanga hivi karibuni wakati wa maonyesho ya
biashara
MENEJA
wa Huduma za Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nelson Mlali amesema
shirika hilo lipo kwenye utaratibu wa manunuzi ya boti ambayo itapita
maeneo mbalimbali kuelimisha jamii ikiwa ni mkakati wa kuzuia vitendo
vya uchafuzi wa mazingira kwenye bahari.
Mlali aliyasema hayo
wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kwenye maonyesho
ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini hapa ambapo
alisema kabla ya mwaka huu kwisha itapatikana ili waweze kushirikiana na
taasisi nyengine.
Alisema taasisi ambazo watashirikiana nazo ni
zile ambazo zinaangalia maeneo hayo kiusalama wa mazingira na pia
kiusalama wa nchi kwa sababu bandari ni mipaka ya kimataifa.
Alisema
kwa Tanzania uchafuzi wa mazingira kwenye pwani yao sio mkubwa kama
zilivyo nchi nyengine huku akibaini changamoto zinazowakabili ni
wananchi kutokufahamu shirika hilo na shughuli wanazofanya kwa sababu
bado ni changa hivyo wapo kwenye utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi.
“Elimu
hiyo itakuwa ni kuhusu biashara za kimataifa kupitia njia za maji
zinazofanyika kwa hivyo tumekuwa tukifanya mikutano mbalimbali ya kuwapa
uelewa mkubwa”Alisema
Hata hivyo alisema uingiaji wa meli
nchini umeongezeka hasa kwa sababu ya madhara yaliyotokana na COVID 19
kwa nchi nyengine ambazo walikuwa wameweka vizuizi lakini kwa hapa
nchini hatukujaweka na hivyo kuruhdu meli kuja kuleta shehena na
kubadilisha mabaharia.
“Meli kutoka Dunia nzima zimekuwa
zikiingia kwa mfano za mafuta zinazotoka ukanda wa Huba zinaleta mafuta
ikiwemo Kuiwati,Saudi Arabia na nchi nyengine nyingi..,Meli za ngano
kutoka Ulaya Mashariki na nyengine dunia nzima”Alisema
Hata hivyo alitoa
wito kwa wafanyabiashara wazingatia masuala ya usalama wanapotumia njia
za usafiri wa majini na wanapopanda vyombo na wanaposafirisha mizigo
huku akiwataka wamiliki wa vyombo wafuate utaratibu.