Kwa kuliona tatizo hilo ambalo linakwamisha maendeleo ya taaluma wilayani Ludewa shirika hilo kupitia mradi wake wa MAMMIE unaotekelezwa katika kata za Mawengi,Milo,Mavala,Lubonde Madope na Luwana likaona ulazima wa kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu wa taaluma kutoka shule 20 za mradi likiwa na lengo la kuondoa kabisa tatizo hilo ,Kama ambavyo Nemes Temba Mratibu wa mradi anavyoeleza.
Awali akifungua mafunzo ya stadi za kusoma,kuandika na kuhesabu,Afisa elimu taaluma mkoa wa Njombe Joseph Lupolo amesema kitendo kilichofanywa na shirika hilo kitaleta mapinduzi kwenye taaluma Ludewa kwasababu kipindi cha nyuma ,moja ya shule za mwambao mwa Ziwa Nyasa kulitokea wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba bila kujua KKK.
Baadhi ya walimu akiwemo Kratianus Johani ambaye ni mwalimu mkuu shule ya msingi Sambala wanasema ujuzi mpya waliopewa utapelekwa ipasavyo kwa wanafunzi na kuondoa kabisa tatizo lililokuwepo kipindi cha nyuma cha kuhitimu bila ya kuwa na ujuzi mzuri wa kusoma,kuandika na kuhesabu.