Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Happiness Seneda akiongea na watendaji wa halmashauri ya Mji wa Mafinga wakati wa baraza maalum la kujibu hoja za CAG
Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi na madiwani wa halmashauri ya Mji wa Mafinga.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
KATIBU tawala wa mkoa wa Iringa amewataka watendaji wa Halmashauri zote za mkoa wa Iringa kujibu hoja za CAG kama walivyo agizwa ili kuondoa maswali ambayo yamekuwa na utata katika utendaji wao wa kazi.
akizungumza kwenye baraza la madiwani la kujibu hoja za CAG katika halmashauri ya Mji wa Mafinga,Katibu tawala Happiness Seneda alisema kuwa watendaji wote wanatakiwa kujibu hoja za CAG kwa kuwa tayari zinaonyesha kuwa kuna mambo ambayo hajaenda sawa ndio maana kuna hoja hizo.
Alisema kuwa watendaji wa halmashauri wanatakiwa kufanya kazi kwa karibu na kutoa ushirikiano kwa wakazi wa ndani na wakaguzi wa nje ili kuhakikisha wanaondoka kabisa hoja ambazo sio za msingi ambazo mara kazaa zinapelekea kupata hadi chafu.
Aidha Seneda alisema kuwa wakurugenzi na watendaji wa Halmashauri kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na kanuni za ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikokea mara kwa mara kama ambavyo watndaji wa chini wamekuwa wakitumia mabavu kuongoza wananchi na kuibua migogoro.
“ukienda huko vijijini au mitaani utajionea namna ambavyo viongozi wetu wanavyoongoza kwa kutumia mabavu bila kufuata sheria za uongozi na kusababisha wananchi kukimbilia katika ofisi ya mkuu wa mkoa kutoa kero zao ambazo zingeweza kutatuliwa huko huko chini” alisema Seneda
Seneda aliwataka watendaji wote wa halmashauri kuhakikisha wanabuni miradi mingine mipya ya kimkati kwa lengo la kuhakikisha wanaongeza kipato cha halmashauri na sio kutegemea kodi tu kila wakati kama ambavyo wanafanya hivi sasa.
Aliongeza kwa kuwataka wametaji kuhakikisha wanasimamia vilivyo miradi yote ambayo inatekelezwa kwenye halmashauri zao kwa lengo la kuendana na thamani ya fedha ambazo zinakuwa zimetumika kwenye miradi hiyo.
Seneda alimalizia kwa kuwataka viongozi wote kupambana kuhakikisha wanapunguza au kuondoa kabisa vifo vya mama na mtoto kwa kuwa swala hilo linawezekana kwa kutoa huduma bora ya afya kwa mama na mtoto.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga alizitaka halamshauri kuhakikisha wanavibana vikundi vyote kulipa mikopo kwa wakati ambayo wamekopa ili kutoa fursa kwa wananchi wengine kunufaika na fursa ya mikopo hiyo ambayo ipo kisheria.
alisema kuwa vikundi vyote ambavyo vimekuwa vikikopa fedha za halmashauri na kutorudisha kwa wakati visikopeshwa tena mikopo hiyo kwa kuwa wanakuwa wamekiuka masharti ya mikopo hiyo.
Sendiga aliwataka wataalam wa tehama kuhakikisha kuwa tatizo la kuharibika kwa mashine za kukusanyia kodi linafanyiwa kazi haraka ili kuepuka kukosa kodi ambazo zinapotea bila sababu yoyote ile.