Mkuu wa wilaya ya Longido,Frank Mwaisumbe akizungumza katika mkutano huo unaoendelea jijini Arusha
Washiriki wa mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Longido ,Frank Mwaisumbe mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo jijini
(Happy Lazaro)
……………………………………………………………………
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Nchi 7 za Afrika zimetakiwa kuwa na mifumo sahihi ya taarifa za barabara itakayosaidia kuokoa fedha za Serikali ili kutambua mahitaji mbalimbali ya ujenzi wa miundo mbinu ya barabara .
Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo,mkuu wa wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe katika mkutano wa siku Saba unaofanyika jijini Arusha ambao umeandaliwa na TARA kwa ushirikiano wa wizara ya ujenzi na International Road Federation (IRF) amezitaka nchi hizo kuja na majawabu sahihi yatakayoondoa changamoto kwenye Mtandao wa barabara katika nchi hizo.
Mwaisumbe amesema kuwa, pamoja na ujenzi ukarabati wa barabara zetu bado suala la takwimu linaonyesha kutokuwepo hivyo kupoteza mapato ya serikali kwa ucheleweshaji wa ujenzi kwa kukosa takwimu sahihi.
“Tanroads Tarura shirikianeni kwa pamoja katika kuondoa changamoto katika mfumo wa taarifa za barabara zetu za ndani kupata taarifa mapema na kuzitatua kabla hazijaharibika utasaidia kuokoa fedha za Serikali”amesema.
Naye Katibu mtendaji wa Shirikisho la barabara nchini Hagai Bishanga amesema kuwa, mafunzo hayo yameandaliwa kwa kushirikiana na wizara ya ujenzi na Uchukuzi na kuzishirikisha nchi 7 ambazo ni Msumbiji Tanzania Zimbabwe Siraleon Liberia Moroco Kenya na Uganda ili kupata uzoefu na kuja na maazimio ya pamoja yatakayopeleke ujenzi wa barabara nzuri za kimataifa.
Amesema kuwa ,bado kumeendelea kuwa na changamoto kubwa ya kukosa taarifa sahihi za mifumo ya ujenzi na ukarabati wa barabara zetu ili kuchochea uchumi wa mataifa yetu ikiwemo kutokuwa na takwimu sahihi ambazo mifumo ya utambuzi na sera zisizokidhi mahitaji.
Akizungumzia changamoto kubwa katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara kuwa ni pamoja na fedha kidogo zinazotengwa ambazo hazikidhi mahitaji , mfano hapa nchini ni fedha inayotengwa ni nusu ya mahitaji yaliokusudiwa.
Bishanga amesema kuwa, changamoto nyingine ni kutokuwa na mifumo sahihi inayotoa taarifa kuhusu matumizi ya barabara bila kuathiri matumizi ya barabara pamoja na sera zilizopo hazikidhi mahitaji.