Home Mchanganyiko TET YAWATAKA WAWEZESHAJI MUONGOZO WA STADI ZA MAISHA KUWA WAZALENDO

TET YAWATAKA WAWEZESHAJI MUONGOZO WA STADI ZA MAISHA KUWA WAZALENDO

0

 

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imewataka wawezeshaji wa Ujaribishaji wa Mwongozo wa kufundisha Elimu  stadi za maisha za afya  ya uzazi ,VVU/ukimwi  na jinsia kwa Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kuwa na uzalendo katika kuifanya kazi yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tazania Dkt. Aneth Komba katika  ufungaji wa  mafunzo hayo yaliyofanyika Mkoani Morogoro kwa siku sita ambapo amewaambia washiriki kuwa mafunzo waliyoyapata  yawe chachu  katika utaoji wa Elimu ya Afya ukiwemo maambukizi ya VVU/UKIMWI, ukatili  na unyanyasaji wa kijinsia nchini.

“Ningependa ifahamike kwa sasa Miongozo hii ipo kwenye majaribio , wawezeshaji wakati mnapofanya ujaribishaji  mnapaswa  kufuatilia na kupata mrejesho ya kipi kinahitajika katika kufanyiwa marekebisho’ amesema Dkt.Komba.

Dkt Komba ameongeza kuwa  TET kwa kushirikiana na Shirika la UNESCO,TACAIDS,Maria Stops na shirika la  Room to Read watafuatilia kwa karibu ujaribishaji wa miongozo hiyo katika halmashauri zote 13 zilizopanga kufikiwa.

Naye mwakilishi  kutoka wizara ya TAMISEMI,Bi.Teresia amesema kuwa  miongozo hiyo  itasaidia  katika kupunguza  au kumaliza kabisa maambukizi mapya  ya virusi vya Ukimwi kwa wahusika watakaopatiwa Elimu hii ya stadi za maisha  itasaidia wanafunzi kuweza kupambana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo wanafunzi wengi kushindwa kumaliza  Shule .

Ameongeza kuwa TAMISEMI imefurahishwa na kuona walimu wengi wameweza kupata mafunzo hayo ambayo kwa vitendo na kuwa kila Shule itaweza kuwa na walimu wawili wawilii kwa Shule za Msingi na Sekondari na wataweza kufundisha stadi za maisha kwa wanafunzi.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku sita  na kuwashirikisha  jumla ya washiriki 46 wakiwemo Walimu ,Maafisa kutoka TAMISEMI,Wakufunzi na Wataalamu wa afya ambapo jumla ya walimu 1696 wa shule za Sekondari na Msingi wanatarajiwa kuwezeshwa kwenye mafunzo hayo kwenye halmashauri 13.