Baadhi ya vijana na wanawake wakipewa elimu kutoka mradi wa kuelimisha vijana na wanawake juu ya
ushiriki wao katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji unaotekelezwa
na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC kwa ufadhili wa internews
Tanzania
Na Fredy Mgunda,Iringa.
VIJANA na wanawake wa kijiji
cha Kidamali kata ya Nzihi mkoani Iringa wanakumbana na vikwanzo vya kupata
elimu ya kufanya maamuzi kwenye mikutano ya serikali za mitaa na vijiji ili
kuchangia shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Wakizungumza mara baada ya kupata
elimu kutoka mradi wa kuelimisha vijana na wanawake juu ya
ushiriki wao katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji unaotekelezwa
na shirika lisilo la kiserikali la IDYDC kwa ufadhili wa internews
Tanzania ambapo baadhi yao walieleza kutokuridhishwa na
utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Walisema kuwa kumekuwa na
utekelezaji wa miradi mingi katika vijiji na mitaa yao ambayo ushirikishwaji
wake umekuwa mdogo kiasi cha vijana wengi kutoshiriki kwa kiasi kikubwa.
Waliongeza kuwa kwenye mikutano
ya hadhara mara kadhaa wamekuwa wakiuliza kuhusiana na jinsi miradi
inavyotekelezwa lakini hawapati majibu yanayojitosheleza kiasi cha kuwakatisha tamaa
vijana na wanawake kuuliza maswali ya mapato na matumizi.
Vijana na wanawake hao walisema
kuwa baada ya kupata elimu kutoka mradi wa kuelimisha vijana
na wanawake juu ya ushiriki wao katika kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa
na vijiji unaotekelezwa na shirika lisilo la kiserikali la
IDYDC kwa ufadhili wa internews Tanzania ambapo baadhi yao walieleza kutokuridhisha
na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao jambo linalopelekea
kuwa na mwamko mdogo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo.
vijana hao walisema kuwa
ushiriki wa vijana na wanawake katika shughuli za maendeleo unapungua siku hadi
siku, kutokana vijana wenyewe kutoona umuhimu wa kushiriki,kutopewa nafasi
ya kudadisi juu ya Miradi ya Maendeleo na kupewa majibu
yasiyoridhisha.
Yeremia Kibasa na winfrida mgovano ni baadhi ya vijana katika
Kijiji cha kidamali walisema wamekuwa wanakumbana na chuki pale ambapo
wanaamua kuuliza maswali ya utekelezaji wa miradi ya kijiji au maswali
yanayohusu suala zima la rushwa na ubadhirifu fedha katika miradi ya maendeleo.
Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa Victor Simon alisema
changamoto ya ushiriki wa vijana na wanawake katika shughuli za maendeleo
hutokana na viongozi katika maeneo mengi kutofuatilia sera ya vijana na wanawake
na kuwajulisha namna wanaweza kunufaika na rasilimali
zilizopo katika maeneo yao.
Naye mdau wa masuala ya maendeleo Mkoani Iringa Juma Makalla alisisitiza
kwamba kutoshiriki katika shughuli za maendeleo kunapelekea vijana wengi kuwa
tegemezi katika jamii na familia.
Mratibu wa mradi kutoka shirika lisilo la kiserikali la Iringa
Development of Youth ,Disabled and children care {IDYDC} Ruben Magayane alisema
kuwa mradi umejikita kuelimisha vijana na wanawake juu ya ushiriki katika
kufanya maamuzi kwenye serikali za mtaa na vijiji ili kuongeza hamasa kwa kundi
la Vijana na wanawake kushiriki katika nyanja mbali mbali.
Magayane alisema kuwa vijana na
wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele
kutumia fursa zilizopo ili kuhakikisha wanachangia katika shughuli za
kimaendeleo za familia na jamiii inayowazunguka kwa kutoa maamuzi yenye faida
chanya na wao sehemu ya wafanyaji maamuzi.