Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Profesa Zacharia Mganilwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi pamoja na wanafunzi wanaosoma kozi ya Urubani katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo mara baada ya kusainiwa Mikataba miwili ya kupeleka vifaa vya kusomea masuala mazima ya Usafirishaji wa ndege pamoja na Vitabu vya sekta ya usafirishaji wa anga, Maji na Reli.
Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya chuo cha NIT, Rukia Shamte, akizungumza wakati wa kusaini mikataba leo katika chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa akibadilishana mkataba na mwakilishi wa kampuni ya Mallory International Limited mara baada ya kusaini Mkataba huo.
Picha ya pamoja.
Mwakilishi wa kampuni ya Mallory International Limited Wakibadilishana mikataba na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Prof. Zacharia Mganilwa mara baada ya kusaini leo katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji.
CHUO cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimesaini Mikataba miwili na wazabuni kutoka kampuni ya Kichina inayojihusisha na biashara ya vifaa vya usafiri wa anga Avic International Holding Company na kampuni ya Mallory International Limited kwa lengo la kununua Vifaa mbalimbali vya mafunzo na vitabu katika chuo hicho.
Mkataba uliosainiwa na Chuo Cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Avic international Holding unaogarimu zaidi ya USD milioni 1.2 ( bilioni 2.4) na ule wa Kampuni ya Mallory wa USD 300,000 000 (Milioni 700) ni sehemu ya kutekeleza mradi unaofadhiliwa na benki ya dunia chuoni hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam leo Juni 5, 2021, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Zacharia Mganilwa amesema kampuni ya Avic, ndio imeshinda zabuni ya kulete vifaa vya kutumika kufundisha wahudumu ndani ya ndege ambapo wahudumu hao watafundishwa usalama wa abiria kwenye ndege pamoja na vifaa vya kufundishiwa wahandisi wa matengenezo ya ndege hapa nchini.
“Vifaa hivi ni vya Kisasa kabisa ambavyo vinatumika duniani kote, Ulaya, Marekani nao wanatumia vifaa kama hivyo.” Amesema Prof. Mganilwa.
Amesema vifaa hivyo vitawawezesha vijana wa kitanzania kusoma hapa hapa nchini ambapo zamani mafunzo hayo walikuwa wakiyafuata nje ya nchi….”vifaa hivyo vikifika vijana wengi watajifunza hapa hapa na kuweza kuendesha mashirika yetu ya ndege kwa usalama na umahiri mkubwa, kuketa faida na kuwahudumia watanzania watakao kuwa wakitumia usafiri wa ndege”.
Aidha amesema, mkataba wa pili waliousaini leo ni kati ya Chuo cha Usafirishaji na kampuni ya Mallory ambayo imeshinda zabuni ya kuwapelekea vitabu ambapo katika mkataba huo kampuni ya Mallory itatoa vitabu elfu 10 chuoni hapo kwa ajili ya kufundishia usafiri wa anga, usafiri wa Maji pamoja na usafiri wa reli.
“Tunatarajia vitabu hivyo vitakuwa katika maeneo ya Usafiri wa Anga, Usafiri wa Maji na usafiri wa Reli ambapo vitawawezesha wanafunzi na watafiti wa masuala ya usafirishaji kuweza kuvitumia na hivyo kuweza kutoa huduma ya kitaalamu katika Chuo Cha Usafirishaji amesema Profesa Mganilwa.
Profesa Mganilwa amesema, upatikanaji wa vifaa hivyo, utasaidia sana katika miradi mbali mbali inayoendelea hapa nchini kwa sasa hasa mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ununuzi na ujenzi wa Meli na ufufuaji wa sekta ya anga ambapo sasa wataalamu wataweza kuwa mahili na baada ya hapo nchi itegeme kuwa na mpango wa uchumi kutoka katika sekta ya Usafirishaji.
Kwa Upande wake Mhandisi wa Ndege na Mkufunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mhandisi Abubakar Noor amesema, mikataba hiyo iliyosainiwa leo wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP) umelenga kukuza vyuo vya Ufundi kuwa vyuo vya umahili.
Mhandisi Noor amesema kupitia mikataba hiyo, Chuo cha NIT kitakuwa na kituo cha Umahili katika anga ambapo watafundisha mafunzo mbalimbali yanayohusiana na usafiri wa anga ikiwemo urubani, uhudumu ndani ya ndege na uhandisi matengenezo ya ndege.
Amesema wanafunzi wataenda kupata uhalisia wa kazi ambazo wanapaswa kuifanya watakapokuwa wameajiriwa katika sekta ya usafiri wa anga.
“Tunatarajia mafunzo haya tutayafundisha kwa kiwango au kwa ngazi ya PPL. ambayo ni Private Pilot Licence, mafunzo hayo Rubani atapata mafunzo ya awali ya kurusha ndege, pia kutakuwa na mafunzo ya CPL ambayo Comercial pilot Licence ambapo Rubani atapata leseni ya kurusha ndege ya buashara.” Amesema Mhandisi Noor.
Mafunzo hayo yatatolewa mara baada ya kukamilisha kununuliwa kwa ndege ndogo mbili ambapo moja wapo itakuwa na injini mbili kupitia mradi huo wa East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP).
Mhandisi Noor amesema kuwa mafunzo hayo yatatolewa katika Chuo Cha Taifa ya Usafirishaji tuu na sio vyuo vingine.