Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani nkoa wa Iringa MNEC Salim Abri Asas akibandika stika kwenye gari ikiwa ishara ya kuashiria kuwa uzinduzi umefunguliwa rasmiMkuu wa wilaya Richard Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa angalia zoezi la ubandikaji stika kwenye gari ikiwa ishara ya kuashiria kuwa uzinduzi umefunguliwa rasmiMwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani nkoa wa Iringa MNEC Salim Abri Asas akiwa na Mkuu wa wilaya Richard Kasesela sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Juma Bwire pamoja na Meya wa manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada
WANANCHI wa mkoa wa Iringa
wametakiwa kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali
mbalimbali ambazo zimekuwa na kuleta madhara kwa binadamu.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa
kampeni ya safari salama mkoani Iringa,mwenyekiti wa kamati ya usalama
barabarani nkoa wa Iringa MNEC Salim Abri Asas alisema kuwa wananchi wanatakiwa
kuendelea kuzifuata sheria na kanuni za usalama wa barabrani ili kuepusha ajili
barabarani.
Alisema kuwa imezuka tabia ya
madereva wa vyombo vya moto kuvunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi
na kusababisha ajali huku wakiwa wanazitambua sheria hizo.
“Unakuta dereva anajua kabisa anavunja
sheria za usalama barabarani lakini anaendelea kwa makusudi na kusababisha
ajali,rai yangu kwa wananchi wote wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanafuata
sheria hizo za usalama barabarani” alisema Asas
Alisema kuwa kumekuwa tabia ya
matumizi mabaya ya zebra zilizopo mkoani Iringa kwa wananchi kuvuka katika eneo
hilo huku anaongea na simu kuna madereva wa vyombo vya moto ambao nao hukiuka kwa
makusudi sheria za barabarani.
MNEC Asas alisema kuwa imerudi
tabia ya madereva bodaboda kupakia abiria zaidi ya mmoja (Mshikaki) jambo
ambalo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani kwa kuwa inahatarisha usalama
wa wananchi wanaotumia usafiri huo.
“Ukipakia mshikaki kunakuwa na
hatari kubwa ya kupata ajali hivyo lazima madereva bodaboda wafuate sheria za
usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za msingi kwa kuhatarisha maisha
ya binadamu” alisema MNEC Asas
MNEC Asas aliliomba jeshi la polisi
kuendelea kusimamia vilivyo sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali
ambazo zimekuwa zikipoteza maisha ya wananchi wengi bila sababu ya msingi hivyo
jeshi la polisi linamamlaka zote za kuhakikisha sheria za usalama barabarani
zinafuatwa vilivyo.
Alisema kuwa imezuka tabia ya
madereva Bodaboda kuto vaa kofia ngumu kwa makusudi huku wakijua kuwa sheria ya
usalama barabarani inakaza kwa lengo la kuwakinga na ajali ambazo zinazotea
barabarani kwa kuokoa uhai wao.
Meya wa manispaa ya Iringa
Ibrahimu Ngwada alisema kuwa usalama wa raia wa manispaa ya Iringa upo mikononi
kwa wananchi wenyewe kwa kufuata sheria za usalama barabarani ambazo zimekuwa
zikitolewa mara kwa mara na jeshi la polisi mkoa wa Iringa.
Aliwataka wananchi wa manispaa ya
Iringa kuhakikisha wanaulinda uhai wao wanapotumia vyombo vya moto ili kuepusha
ajali ambazo zinaweza kuepukika
Aidha meya Ngwada aliwaomba
wananchi wa Manispaa ya Iringa kuendelea kufanya usafi katika maeneo ya makazi
na maeneo ya biashara ili kuepusha kukumbwa na magonjwa ya milipuko ambayo inazuilika.
Ngwada aliwaomba wananchi
wanaofanya shughuli za kibiashara pembezoni mwa barabara wanatakiwa kutafuta
njia mbadala ya kujiepusha na ajali za barabarani kwa kufuata sheria za usalama
barabarani ili kuulinda uhai wao.
Ngwada alimalizia kwa kuwaambia
wananchi wa manispaa ya Iringa kuwa wameanza kutafuta njia mbadala wa
kutengeneza barabara zote ambazo zimeharibika kwa kuwa zimekuwa kero kwa
watumiaji wa njia hizo.
Naye kamanda wa polisi mkoa wa
Iringa ACP Juma Bwire alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi wa kwanza hadi mwezi
wa tano kumetokea ajali kumi na saba (17),vifo kumi na tano (15),watu
waliofariki walikuwa wanaume tisa (9),wanawake sifuri (0) ajali za majeruhili
zilikuwa mbili (2),watu waliojeruhiwa walikuwa wanaume kumi na moja(11) na
wanawake watatu (3).
Alisema kuwa mwaka 2021 jumla ya
ajali zilikuwa kumi na nne (14) pungufu kwa ajali tatu saw ana asilimia 18%
ajali za vifo zilikuwa nane ambapo pungufu kwa asilimia 11%,waliofariki
walikuwa wanaume nane na hakuna mwanamke hata mmoja,ajali za majeruhi zilikuwa
sita nalilikuwa ongezeko la majeruhi wane na wanaume waliokuwa wamejeruhiwa
walikuwa kumi na tano (15) na wanawake walikuwa tisa (9).
ACP Bwire aliwataka wananchi
kuendelea kutoa taarifa za uharifu na wahalifu na kuendelea kutii sheria bila
shuruti ili kudumisha amani ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa ujumla.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya Richard
Kasesela ambaye alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa
aliwataka wakandarasi wanaopewa tenda ya kutengeza barabara kuhakikisha
wanazingatia sehemu ya watembea kwa miguu ili kuepusha ajali ambazo sio za
msingi.
Kasesela alisema kuwa barabara
mpya zinazojengwa hivi sasa zinatakiwa kuzingatia watembeaji wa miguu,watu
wenye ulemavu zinatakiwa kuwekewa alama ambazo zitawasaidia kuepusha ajali za
barabarani.
Aliliagiza jeshi la polisi mkoa
wa Iringa kuhakikisha wanawakamata madereva bodaboda wote wanaoendesha chombo
hicho huku wakiwa wamevaa ndali kwani ni kinyume cha sheria za usalama
barabarani.
Kasesela ameugiza uongozi wa halmashauri
ya manispaa ya Iringa kurekebisha barabara ya zizi ili kuepusha ajali na foleni
ambayo huwa inatokea katika barabara hiyo na kuwataka jeshi la usalama
barabarani kuwachukulia hatua kali wanaovunja sheria za usalama barabarani ili
iwe onyo kwa wananchi wangine.