Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa Kati Kati akiwa na baadhi ya viongozi wa Chama alipokwenda kuwatembelea wahanga ambao nyumba yao iliungua kwa Moto katika kata ya kongowe.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wa kulia akiangalia shule ya msingi Muungano ambayo ilichomwa na Moto na watu wasiojulikana.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
******************************
NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Mjini Mhe Silyvestry Koka amefanya ziara ya kutembelea shule ya msingi Muungano iliyopo kata ya Kibaha ambayo ilizingua baada ya kuchomwa Moto na watu wasiojulikana na kusababisha hasara kubwa.
Afisa mtendaji wa mtaa wa kwamfipa Bw Kuboja Majogoro amethibitisha kutokea kwa tukio Hilo na kumweleza Mhe Mbunge kuwa kwa kushirikiana na wananchi walifanya jitihada kadhaa za kunusuru Mali lakini walishindwa.
Aidha mtendaji huyo alibainisha kuwa pamoja na kuwaita jeshi la zimamoto lakini tayari jengo la madarasa mawili yalikuwa yameshaungua pamoja na ofisi ya walimu ilikuwa imeshaungua.
Kufuatia kutokea kwa kanga Hilo la moto Mbunge huyo alifanya ukaguzi katika jengo Hilo na kushuhudia uharibifu uliojitokeza na kubainisha kuwa tayari Halmshauri ya mji kibaha imeshaingiza kiasi Cha shilingi milioni 19,200,000/- kwenye akaunti ya shule kwa ajili ya ukarabati umeshaanza.
Katika kukiona Hilo na kuunga juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya elimu Mbuko Koka ameahidi kutoa ushirikiano wa Hali na Mali na kuahidi kuchangia madawati 20 katika shule hiyo ili kuweza kuwapa fursa wanafunzi kuendelea na masomo yao.
Wakati huo huo Koka ametembelea wahanga wa ajali ya moto kata ya kongowe iliyopelekea familia moja kumpoteza kijana wa miaka 22.
Koka akitoa salamu zake za rambirambi amewaomba ndugu jamaa na marafiki pamoja na wafiwa kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu Cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.
Kufuatia matukio hayo ya moto mbunge akiwa ziarani humo alimpigia simu OCD Kibaha kujua kuna mkakati gani wa kuimarisha ulinzi pamoja na kuwaelimisha wananchi kuwa na ulinzi shirikishi.
Pia Koka amelaani vikali vitendo vya baadhi ya wananchi kuvunja Sheria kwa kuamua kwenda kuchoma Moto katika maeneo ya shule pamoja na makazi ya watu kitu ambacho kinarudisha nyuma juhudi za kuleta maendeleo na kuwaomba wananchi kuwafichua watu hao ili waweze kuchukuliwa hatua Kali.