Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, mkoa wa kilimanjaro,Lengai ole Sabaya (34) na walinzi wake watano leo wapandishwa kizimbani mbele ya mahakimu wawili na kusomewa mashitaka sita ikiwepo ujambazi wa kutumia silaha ,utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.
Waendesha mashitaka wa serikali.Tumaini Kwema, Abdallah Chaula na Tresla Garvas mbele ya hakimu mfawidhi Martha mahumbuga na Hakimu mkazi Mkuu Salome Mshasha walisema Sabaya na wenzake walitenda makosa hayo januari 20 mwaka huu na Februari 9,2021.
Mwendesha mashitaka Mkuu,Kweka alisema Sabaya anatuhumiwa kuunda genge la uhalifu na kutenda makosa ya uhujumu uchumi na kujipatia fedha kwa njia ya rushwa.
Ilielezwa ilijipatia fedha kiasi cha sh 90 million kutoka kwa mfanyabiashara Fransis Mroso mkazi eneo la kwa Mrombo ambaye alikuwa anatuhumiwa kwa makosa ya ukwepaji Kodi ili amsaidie jambo ambalo ni makosa.
Makosa hayo alitenda na walinzi wake hao akiwepo,John Aweyo maarufu Kama Mike One,Enock Mnkeni(41).
Katika makosa ya unyang’anyi wa kutumia Silaha Sabaya anashitakiwa na walinzi wake pia wawili Sylivester Nyengu(26) maarufu kicheche na Daniel Mbura(38) walitenda kosa la ujambazi wa kutumia silaha Februari 9, baada kumfunga pingu na kumpiga Bakari Msangi ambaye ni diwani wa CCM kata ya sombetini na kumwibia sh 390,000.
Katika tukio hilo lililotokea eneo la Bondeni jijini Arusha wakitumia silaha Sabaya na walinzi hao pia wanatuhumiwa kumpiga mateke na kumtishia silaha na kumpora simu na fedha sh 35,000 Ramadhani Ayoub.
Kwa kuwa makosa hayo hayana dhamana watuhumiwa hao walipelekwa mahabusu gereza kuu la Kisongo hadi June 18 kesi itakapotajwa tena.