Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile wakati alipowasili kwa ajili ya kutembelea vyombo vya habari vya IPP.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akipokelewa na uongozi wa The Guardian Ltd wakati alipokuwa natembelea kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa studio za ITV.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitambulishwa baadhi ya vipindi vya Capital radio
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akielea jambo wakati alipokuwa katika studio za East Africa radio jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Gazeti la Nipashe, bb. Beatrice Bandawe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akielezewa jinsi habari na vipindi mbalimbali vinavyotayarishwa katika studio za ITV. Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One, Joyce Mhavile.
*****************
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) ametembelea vyombo vya habari vya Kampuni ya IPP Ltd na kuvipongeza kwa kufanya kazi vizuri.
Balozi Mulamula ametembelea ‘The Guardian Ltd’ inayozalisha magazeti ya The Guardian na Nipashe, Radio One, Capital radio, East Africa radio, ITV, Capital TV pamoja na East Africa TV.