katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango Emmanuel Tutuba akifunga kongamano la mwaka la usimamizi katika ununuzi wa umma lililofanyoka mkoani Arusha
Mkurugenzi wa TEMESA Martin Kasambala akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kuongamano hilo ambalo taasisi hiyo ilikuwa ni mojawapo ya watoa mada.
Afisa mkuu wa mawasiliano wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania {TPA} Beatrice David Jaivo akiongea na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kongamano la 8 la usimamizi wa ununuzi wa umma ulioandaliwa na malmlaka ya udhibiti ununuzi wa umma [PPRA]
Baadhi watendaji wa taasisi za ununuzi walioshiriki kongamano lao la 8la mwaka usimamizi wa ununuzi wa umma wakiwa katika picha ya pamoja na katibu mkuu wa wizara ya Fedha na Mipango Emmanuel Tutubi mkoani Arusha.
…………………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Katibu mkuu wa wizara ya fedha Emmanuel Tutuba amesema kuwa watendaji wa taasisi za ununuzi wanawajibu wa kutumia nafasi zao katika kulisaidia taifa kwa kuweza kupata thamani halisi ya fedha katika manunuzi wanaoufanya.
Tutuba aliyasema hayo wakati akifungua kongamano la 8 la mwaka la usimamizi katika ununuzi wa umma lililofanyika mkoani Arusha kwa uliondaliwa na mamlaka ya udhibiti ununuzi wa umma (PPRA) ambapo aliwataka kila mmoja kuendelea kujitadhimini na kujua mchango wake ni upi kwa taifa.
Alisema kuwa anaamini siku hizo tatu zimekiwa za tija na zitaleta mabadiliko katika kazi zao ambapo kama viongozi wanatakiwa kuendelea kupanda mbegu njema ya uadilifu ili kuweza kufikia malengo endelevu.
Alifafanua kuwa kama wizara ya fedha na serikali kwa ujumla wanalojukumu la kuangalia eneo hilo la ununuzi kwani karibia asilimia 80 ya bajeti inatumia katika eneo hilo.
Aidha kuhusiana na mfumo wa TANePS alisema kuwa pamoja na faida zake Kuna wakati wanatumia lakini bado bei zinakuwa juu hivyo ni vizuri wakautumia kulingana na mazingira halisi ambapo pia alisema hadi sasa kuna sehemu ambazo bado hawajaanza kutumia mfumo huo kwa kuona kuwa utawazibia kupata fedha.
“Mkitumia taratibu, sheria na miongozo vibaya mnaweza mkatumia rasilimali za nchi vibaya hivyo nataka nafasi zenu ziwasute mkafanye jambo sahihi kwa manufaa ya nchi yetu lakini pia mjadili BOQ kabla ya kwenda kwenye ununuzi ili kama kuna aliyeingiza jambo kwa maslahi yake binafsi muweze kugundua na kuzuia,” Alisema Tutuba.
“Kahakikisheni mnasimamia kila kipengele kama kinavyohitajika lakini pia katumieni elimu na ujuzi mliyoipata kwa maslahi ya taifa na mtakaporudi katika maeneo yenu ya kazi mkasimamie vizuri mfumo wa TANePS lakini pia mkawashirikishe na wengine mliowaacha maofisini ili wote mkawe na uelewa wa pamoja,” Alisema.
Pia aliwataka kuacha mgongano wa maslahi na kwenda kuongeza uwazi, ubora wa kazi na kuhakikisha wanazingatia taratibu ili waweze kuepuka vitendo viovu vya RUSHWA.
Emmanuel Urembo mmoja wa washiriki kutoka tume ya uchaguzi[NEC] akizungumza kwa niaba ya washiriki ambao walikuwa 378 alisema kuwa wamepokea maelekezo yote na wataenda kuyatekeleza na kuwa chahu ya mabadiliko katika taasisi zao.
Kwa upande wake Martin Kasambala mkurugenzi wa TEMESA alieleza kuwa bado watu wanalalamikia taasisi hiyo kutofanya vizuri lakini ni kutokana na mdeni makubwa wanayozidai tasisi hizo kwa muda mrefu jambo ambalo linazuia maendelo ya TEMESA.
“Wanaleta magari tunayatengeneza zaidi ya mara moja wanayachuku lakini hawalipi kwa wakati, tunadai zaidi ya bilioni 22 na tumeshawasilisha hili wizarani ila tunashauri kuwe na mfuko hazina ambao utakuwa ni kwaajili ya kutengeneza magari, wao wakileta magari kwetu sisi tunayatengeneza alafu hazina wanatulipa, hii itasaidia kuondoa changamoto hii na kuifanya TEMESA ikue,” Alisema Kasambala.
Naye afisa mkuu wa mawasiliano wa mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania {TPA} Beatrice David Jaivo alisema kuwa kufuatia kongamano hilo wameweza kupata elimu mbalimbali itayosaidia kusukuma tasnia ya ununuzi mbele pamoja na maendeleo ya taifa hasa katika suala zima la kutumia mfumo wa TANePS .
“Nashauri taasisi ambazo bado hazijanza kutumia Mfumo huu waanze watoke kwenye uzamani wa kutumia makaratasi waanze kutumia mfumo na waendane na teknolojia na hii itasaidia kuondoa urasimu,” Alisema Bi Jaivo