Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe,akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Pyxus kilichopo Kizota kinachozalisha mafuta ya kula ya Alizeti leo Juni 2,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya wazalishaji wa Mafuta ya kula ya Alizeti wakimsikiliza Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe (hayupo pichani) akizungumza mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Pyxus kilichopo Kizota kinachozalisha mafuta ya kula ya Alizeti leo Juni 2,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
KATIKA kutatua changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini serikali imejipanga kutatua changamoto ya upatikanaji wa mbegu bora ya alizeti kwa kushirikiana na viwanda vya uzalishaji mafuta ya kula.
Hayo amesemwa leo Juni 2,2021 jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe. alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha Pyxus kilichopo Kizota .
Mhe.Bashe amesema kuwa viwanda vya mafuta ya kula kikiwemo cha Pyxus vinatakiwa kuendelea kuifanyia majaribio mbegu ya alizeti aina ya Record iliyotolewa na Wakala wa mbegu nchini (ASA) ambayo imeanza kuonyesha matokeo chanya katika uzalishaji wa zao la alizeti.
“Pyxus wametupa uzoefu kutambua kwamba mbegu inayozalishwa na Wakala wa Mbegu (ASA) iitwayo Record ina taswira ya kuonyesha matokeo mazuri”amesema Bashe.
Bashe amesema amewahakikishia wazalishaji wa mafuta kuwa inatilia mkazo hasa katika kipaumbele cha kutatua changamoto ya mafuta ya kula kupitia zao la alizeti.
“Nchi yetu ina upungufu wa tan 400,000 za mafuta ambazo tunahitaji tupate mbegu za kuingia kiwandani zaidi ya tani milioni 1.3”amesema Bashe
Kiwanda kama PYXUS kinahitaji tani 20,000 ili kiweze kufanya kazi mwaka mzima,lakini kiuhalisia anapata tani 10,000 hadi 12,000 hawapati mahitaji yao yote.
Tunapohitaji milioni 1.3 ili viwanda vyote nchi viweze kuzalisha mafuta inamana tutahitaji mbegu za kwenda shambani ili kutosheleza uhitaji wa mafuta wa tan
Kwa sasa tani zinazozalishwa ni 620,000
Ili tuzalishe tani 1.3 za kwenda kiwandani tunatakiwa kujua tunahitaji mbegu kiasi gani za kwenda shambani
“Moja ya kampuni ambayo inafanya a very good model ni PYXSUS inafanya kitu kinaitwa contract farming ,kwa hiyo tumekuja kuwahakikishia kwamba serikali imechagua mikoa ya kipaumbele ambayo ni Dodoma,Singida,Simiyu ambayo inayozalisha mafuta ya alizeti
Hata hivyo amewahakikishia kuwapatia mbegu wanazohitaji kwenda kuwagawia wakulima wao ili waweze kuzalisha mbegu za kuingia kiwandani na kiwanda kifanye kazi mwaka mzima .
Lakini pia tunawahikishia kuwa hakutakuwa na zuio la kuuza nje ili wakipata masoko ya nje waweze kuuza nje wakipata soko.
“Zaidi ya asilimia 98 ya mafuta wanayozalisha wanauza nchini na tumeangalia uwekezaji wao na wametueleza changamoto zao ikiwemo bei ya mbegu”amesema
Hata hivyo alisema kuwa Juni 13 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa na mkutano mkoani Singida ambao utahusisha wazalishaji wa mafuta ya alizeti.
“Nchi yetu inahitaji mafta tani 400,000 lakini viwanda vinafanya miezi mitatu tu hakuna mbegu za kutosha kwa sababu waklima hawalimi kwa kutumia mbegu bora na bei mbeg bora ni ghali sana”amesema
Kwa hiyo tutatengeneza mfumo wa financing ambao sisi wizara tutashirikiana na wanunuzi na wasambazaji wa mbegu na tutakaa na ili gharama ya mbegu isibaki kwa mzalishaji
Short time tutanunua kile kilichomo ndani na tutaagiza nje na hii itakuwa ni kwa muda wa mwaka mmoja hadi miwili baada ya hapo tutakwa na uwezo wa kuzalisha mbegu nzuri
Naye Mkuregenzi Mtendaji wa Pyxus amesema kuwa moja ya changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na upatikanaji wa mbegu bora kwa ajili ya kwapatia wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija
Aidha ametumia fursa hiyo kuishukuru Serikali kwa kuweza kutoa ushirikiano katika kutatua changamoto zinazowakabili wazalishaji wa mafta nchini.