……………………………………………………………….
Na.Mwandishi wetu,Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan antarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa nne wa kitaifa wa Tanzania prayer breakfast utakaoshirikisha viongozi mbalimbali wa Kiserikali,wakiwemo mawaziri, manaibu waziri na Makatibu wakuu pamoja na viongozi wanchi nyingine ili kuzungumza masuala ya uongozi,utawala bora maadili na uadilifu katika uongozi utakaofanyika June12 Jijini Dodoma.
Hayo yameelezwa hii leo Juni 2,2021 Jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kingdom Leadership Network Tanzania,(KLNT) Isack Mpatwa wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema mkutano huo utawashirikisha zaidi ya Viongozi wa Kitaifa 500 huku viongozi wa Nchi za nje wakihudhuria kwa njia ya mtandao.
Mpatwa amesema kuwa lengo la Mkutano huo ambao unabebwa na kauli mbiu isemayo utawala bora na uadilifu katika uongozi ambayo inaendana na mtazamo wa Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu inafuata misingi ya utawala bora,uadilifu na kufuata sheria ambayo ndio msingi wa kiuchumi unaowajali wananchi.
“Uongozi wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan una mtazamo katika kutilia mkazo suala la utawala bora na uadilifu ambao ndio msingi wa Sheria na Mkakati wa maendeleo wa Taifa wa 2021 hadi 2025 unasema suala la utawala bora na kufuata sheria ndio nguzo bora ya maendeleo,”amesema.
Katika hatua nyingine amesema kuwa watakuwa na jukwaa kubwa la kibiashara ambalo watalitangaza na litaanza Mwezi wa 10 Mwaka huu ikiwemo Uzinduzi wa Taasisi ya kulelea mawazo ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo na wakati wa Kitanzania lengo ni kuona jinsi gani ya kuweza kukuza mawazo yao katika kukuza biashara zao.
“Tutazindua Mradi mkubwa wa kibiashara baina ya Tanzia na Marekani kuhusu biashara pamoja na kituo cha kulelea mawazo ya kibiashara kwaajili ya kutatua matatizo ya wananchi ambapo hadi sasa tulishafungua chuo cha kibiashara ambacho kinaendelea”,.
tumealika Taasisi za kibiashara na viongozi mbalimbali wa Serikali na msemaji Mkuu atakuwa kubadilishana mawazo ya kibiashara na namna ya kukuza mitaji na mfanyabiashara mkubwa kutoka marekani Bill wiston ndio atakuwa msemaji mkuu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Kingdom Leadership Tanzania, Lewis Kopwe amesema pamoja na mambo mengine watazungumza na viongozi wa kidini,pamoja na wafanyabiashara na mkutano huo unafanyika katika nchi mbalimbali Duniani.
“Mwaka huu tutatoa fursa ya ushiriki wa wananchi kupitia mitandao ya Kijamii ili kufuatilia mkutano huo ambao pia utaambatana na maombi ya kuiombea Nchi ambao utaongozwa na viongozi mbalimbali wa Kidini”,.