Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na wakuu mbalimbali wa Taasisi akiwemo Kamishina wa Makosa ya jinai nchini DCI pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum) Mhe.George Mkuchika hafla iliyofanyika leo June 2,2021 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
…………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Chamwino
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan amewataka Makatibu Tawala wa Mikoa kwenda kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria kwa kusimamia haki kwa kutatua kero za wananchi.
Rais Samia ametoa maagizo hayo leo June 2,2021 Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma mara baada ya kuwaapisha Makatibu Tawala wa Mikoa pamoja na wakuu mbalimbali wa Taasisi akiwemo Kamishina wa Makosa ya jinai nchini DCI pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum) Mhe.George Mkuchika
Aidha amewataka kwenda kufanya kazi kwani Majukumu yaliyo mbele yao ni makubwa wao pia ni Makatibu wa Kamati za usalama za Mikoa hivyo wanatakiwa kuwashauri wakuu .
“Nimewateua sio kuwa mkawe ndio kikwazo Cha kukwamisha maendeleo au kulumbana nyie kwa nyie hapana Nchi hii itajengwa na mtanzania yeyote bila kuangalia katoka wapi sasa mkuu wa mkoa wa Iringa najua utakuwa nakazi kubwa lakini nikutoe hofu nenda kachape kazi,”amesema Rais Samia
Hata hivyo amesema kuwa hatavumilia viongozi wanaodhulumu mali za wananchi ikiwemo kujimilikisha ardhi na kuwapola wananchi maeneo yao kwa nguvu.
“Kuna baadhi ya viongozi walifika katika maeneo yao yakazi wao ndio wanakuwa wakwanza kujimilikisha ardhi badala ya kutatua migogoro sasa sitalifumbua macho Hilo swala hata kidogo,”amesema Rais Samia.
Pia amekemea tabia ya uonevu makazini kuanzia ngazi za mikoa na kuagiza hali hiyo iachwe Mara moja kwani Sheria za kazi haziruhusu vitendo vya uonevu makazini wafanyakazi wote wanalengo moja la kuwatimikia wananchi na kuleta maendeleo nchini.
Mhe Rais Sami amewaagiza wakafanye ubunifu wa vyanzo vya mapato yake ya ndani na kutengeneza fursa kwa wawekezaji zaidi kuwekeza nakuachia kuwasumbua katika kupata vibali na maeneo kama yapo wapewe kwa haraka ili uchumi wa nchi ukue.
“Kazi yenu kubwa ni kusimamia vizuri mapato ya Serikali nakuongeza mbinu za kuongeza wawekezaji ili kuhakikisha Pato la Taifa linaongezeka na si vinginevyo,”ameongeza Rais.