MWENYEKITI wa Kikundi cha Tusumuke Christopher Dioniz,akitoa maelezo kwa wananchi aliyetembelea banda lake la Kuku wakati wa kuhitimishwa kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
MWENYEKITI wa Kikundi cha Tusumuke Christopher Dioniz ameiasa jamii kujenga utaratibu wa kushiriki maonyesho ili kuongeza ujuzi kupitia teknolojia mbalimbali zinazotengenezwa na wabunifu hapa nchini.
Dioniz amesema wakati wa kuhitimishwa kwa maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yaliyokuwa na lengo kuonyesha bidhaa za elimu ya ufundi, yaliyomaliza leo Juni 2,2021 katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Mwenyekiti huyo ambaye kikundi chake kinajishughulisha na ufugaji pamoja na utotoleshaji vifaranga vya kuku amesema,maonyesho yanasaidia kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya ufugaji lakini pia huleta ari zaidi kwa wanaopenda masuala ya ubunifu.
“Kwa mfano hapa kwenye banda letu,tumetengeneza banda la kuku kwa namna ya ubunifu ambayo humwezesha mwananchi kufuga kuku wake vizuri bila shida yoyote.” Amesema Dioniz
Aidha amesema kikundi hicho kimeshiriki maonyesho hayo ili kutoa Elimu kwa wajasiriamali hasa wanaopenda shughuli za ufugaji na utotoleshaji vifaranga vya kuku.
Maonesho ya Pili ya Elimu ya Mafunzo na Ufundi yamefanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma kuanzia Mei 27 hadi Juni 2, 2021 na yameshirikisha Taasisi 151. Kauli mbiu ya Maonesho hayo ni “Kuimarisha Ushirikiano na Wadau katika Kukuza ujuzi kwa Maendeleo ya Viwanda”