Dkt. Minani Ntahosanzwe Mhadhiri wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii akizungumza na wateja waliofika katika banda la Taasisi kupata huduma Katika maonesho ya Pili ya Vyuo vya elimu ya ufundi stadi katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
……………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu,Dodoma
CHANGAMOTO kubwa inayosababisha wanandoa kupeana talaka ama wanawake kutelekezwa na watoto ni wanandoa kutojua misingi ya ndoa imeelezwa
Nchini Tanzania, Utafiti wa kufuatilia kaya Tanzania, wa mwaka 2014/15 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaonyesha kuwa kiwango cha talaka kimeongezeka kwa asilimia 1.1
Mhadidhiri Msaidizi Idara ya Ustawi wa Jamii kutoka Taasisi ya Ustawi wa Jamii Catherine Manda amesema watu wengi wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawajui misingi na maana ya ndoa matokeo yake wanaingia kwenye ndoa na baada ya muda mfupi huachana na kusabisha adha kubwa kwa watoto ikiwemo kukosa haki zao msingi ikiwemo kukosa elimu pamoja na kukosa haki ya kupata upendo wa pande zote mbili.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii jijini Dodoma kwenye maonyesho ya pili ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yaliyoandaliwa na Baraza la Taifa la Vyuo vya Ufundi (NACTE ) na Taasisi ya Sekta Binafsi(TPSF) amesema hali hiyo imekuwa ikisababisha migogoro ya ndoa ambayo kimsingi wanandoa hawana mbinu sahihi ya kuitua na hivyo kusababisha wanandoa kupeana talaka.
Alisema jamii inapaswa ijifunze mbinu za kutatua migogoro na izitumie kwenye familia zao hasa kuzungumza na vijana wao kuhusu mahusiano tangu wakiwa nyumbani ili wakati ukifika wafanye maamuzi sahihi na kuwa na familia bora.
“Migogoro ipo na itakuwepo ,kikubwa tunatakiwa tuwe imara kuboresha mbinu za kuitatua kistaarabu kabla ya kuachana.” Alisema na kuongeza kuwa
“Migogoro ina upande hasi chanya hivyo lazima tugombane lakini pia lazima tupatane maana hapo sasa tunaboresha mahusiano kupitia migogoro.”
Aidha alisema katika utoaji elimu kwa jamii hasa inayoizunguka taasisi hiyo wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa ya wanandoa wengi kutojua misingi na maana ya ndoa lakini pia hawana mbinu wala elimu ya kusuluhisha migogoro ya ndoa na kusababisha kuachana.
“Tunavyoona sisi tunaokutana na hizo kesi watu wengi hawajui misingi ya ndoa ,wanaingia kwenye ndoa wakiwa hawajui misingi na maana halisi ya ndoa lakini pia hawana mbinu wala elimu ya kusuluhisha migogoro.”
Alitumia fursa hiyo kuwaasa wana ndoa kwenda mapema kwenye maeneo husika kutafutana suluhu za ndoa basal ya kufikiria talaka kuwa ndio suluhisho.
“Tunapopita kwa jamii kutoa elimu tunakutana na wanandoa na wengine wanakuja ofisini,tunazungumza nao kuhusu mahusiano ,lakini changamoto ni kwamba ukiona mtu mpaka anaongea ujue mambo yameshakuwa makubwa na wakati mwingine yameshafikia hadi kwenye talaka.” Alisema Manda
Hata hivyo alisema wapo baadhi wanaofanikiwa kurudisha mahusiano yao lakini wengi wao wanakuwa wameshafikia hatua mbaya.
Vile vile alisema kitu kingine kinachosababisha migogoro ya wanandoa ni mawasiliano huku akisema eneo hilo pia kina changamoto kubwa.
” Tunayo program yetu ya ushirikishwaji wa jamii ambapo tunaenda moja kwa moja mitaani kwa kishirikiana na uongozi wa serikali za mitaa kuhakikisha tunasikiliza na kushirikiana nao katika kuzitatua.”
Vile vile akisema changamoto nyingine inayosababisha talaka kwa wanandoa ni mawasiliano kati ya mke na mume.
“Yaani kwa mfano kuna jambo umelipata au umelisikia juu ya mwenzio unaliwasilishaje labda mwenzio kakuudhi,unamwambiaje au unaliwaliwasilishaje kwa mwenzio ili uweze kupata ukweli,katika eneo hili hakuna mawasiliano sahihi”