Naibu katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango Khatib Kazungu akifungua kongamano la 8 la PPRA kwa niaba ya waziri wa fedha na mipango Dkt Mwigulu Nchema.
Afisa mtendaji mkuu wa PPRA Mhandisi Leonard Kapongo akiongea wakati wa ufunguzi wa kongamano lao lililofanyika mkoani Arusha.
Baadhi ya watendaji wa taasisi za ununuzi wa umma wakifuatilia yanauoendelea katika kongamano lao la 8 lililofanyika mkoani Arusha.
******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Naibu katibu mkuu wa wizara ya fedha na mipango Khatib Kazungu amewataka watendaji wa Tasisi za serikali kuwa waadilifu na kujiepusha na vitendo vya Rushwa,ubadhilifu na udanganyifu katika mchakato wa ununuzi.
Kazungu alitoa wito huo wakati akifungua kongamano la 8 la mwaka la usimamizi katika ununuzi wa umma lililofanya na mamlaka ya kudhibiti ununuzi wa umma (PPRA) kwa niaba ya waziri wa fedha Dkt Mwigulu Nchemba ambapo alisema kuwa watendaji hao wanawajibu wa kuhakikisha wanafanya kazi ya ununuzi kwa uzalendo na kuepuka vitendo vyote vinavyoweza kuondoa upatikaji wa thamani halisi ya fedha.
Alieleza kuwa ununuzi ni moja ya majukumu makubwa katika taasisi za umma ambapo ni wazi kuwa jukumu hilo linakabiwa na changamoto nyingi lakini wanapaswa kufanya tathimini ya mafanikio na changamoto hizo hasa baada ya mfumo wa ununuzi wa umma kufanyiwa maboresho mbalimbali ili kuhakikisha kuwa sekta hiyo inachangia ipasavyo katika harakati za ujenzi na maendeleo ya taifa.
“Ni wazi kuwa nyote mliopo hapa mnahusika katika kutekeleza shughuli za ununuzi katika taasisi zenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma na mnao wajibu wa pamoja ya kuhakikisha kwamba michakato hiyo mnaifanya kwa uzalendo, uadilifu na ufanisi mkubwa ili fedha zinazotumika ziweze kuleta manufaa kwa walengwa ambao ni wananchi kwanj wanatarajia huduma zilizo bora na kwa gharama nafuu,” Alisema Kazungu.
Aidha aliwataka watendaji hao kutotumia sheria ya ununuzi kama kichaka cha kukwamisha miradi miradi ya maendeleo bali kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbalj ya maendeleokutoka na umuhimu wa sekta hiyo.
“Ni ukweli usipingika michakato ya ununuzi katika taasisi zetu inapaswa kuendeshwa na kusimamiwa kwa kuzingatia misingi ya uadialifu, uwazi na haki ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha inapatikana kwenye ununuzi huo lakini pia ni sehemu mojawapo ya kuunga juhudi za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Rais Samia Suluhu ambayo imeeleza wazi mipango madhubuti ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa lengo la kuwaletea wananchi maendeleo endelevu,” Alieleza.
Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa PPRA Mhandisi Leonard Kapongo alisema kuwa katika kongamano hilo watapata elimu juu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na nyenzo na miongozo ya ununuzi wa umma inayotolewa na serikali na hayo yote hufanyika ili kuhuisha upqtikani halisi wa thamani ya feha kwenye ununuzi wa umma.
“Ili kufikia azma hii ni muhimu wadau wote wawe na uelewa wa pamoja wa sheria ya ununuzi wa umma na kuizingatia ambapo tukiyafanya yote ipasavyo mfumo huu utaendelea kuwa na tija na kutafsiri thamani halisi ya fedha,”Kapongo.
Mhandisi Kapongo alisema kuwa kongamano hilo linafanyika baada ya kutoa mafunzo ya sheria kwa ya ununuzi wa umma kwa watendaji 2,300 kutoka tasisi za ununuzi 310 ambapo pia wametoa mafunzo ya mfumo wa ununuzi wa njia ya mtandao (TANePS) kwa washiriki 239 ikijumuisha mafunzo maalum kwa taasisi nunuzi 557 sawa na asilimia 98.
“PPRA inaendelea kuweka juhudi katika kuhakikisha kuwa taasisi zote za ununuzi zinaunganishwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na asilimia 2.3 ya taasisi ambazo hazijaunganishwa kwenye mfumo,” Alisema.
Naye Profesa Sufiani Bukurura akimwakilisha mwenyekiti wa bodi ya PPRA alisema kuwa kongamano hilo lenye kauli mbiu “maboresho ya mfumo wa ununuzi wa umma nchini: mafanikio na changamoto” inalenga inalenga kuwapa fursa wadau ya kujitathimini wenyewe kuhusu mafanikio na changamoto baada ya maboresho mbalimbali ambayo yamefanywa katika sekta ya ununuzi wa umma ikiwa ni pamoja na matumizi ya mfumo wa ununuzi wa umma kwa njia ya mtandao(TANePS).
Pia Profesa Bukurura aliiomba wizara na serikali kwa ujumla kuwaongezea bajeti na kuwawezesha kupata watumishi wa kutosha kwani hadi sasa idadi iliyopo ni nusu ya idadi inayohitajika kwa mujibu wa ikama yao.