Shirika lisilo la Kiserikali la Agri Thamani Neema Lugangira ambaye pia ni MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo |
WABUNGE wameishauri Serikali kurudisha mashuleni somo la sayansi kimu
ili watoto wafundishwe kuandaa lishe bora tangu wakiwa watoto, jambo
ambalo litasaidia kupambana na athari zitokanazo na lishe duni.
Akizungumza
katika semina lishe kwa Umoja wa Wabunge Wanawake (TWPG), iliyoandaliwa na
Shirika lisilo la Kiserikali la Agri Thamani, Mbunge wa Urambo (CCM) Magareth
Sitta alisema zamani watoto walifundishwa juu ya kutayarisha chakula lakini
hivi sasa hawajifunzi tena.
“Serikali
kwanini wameondoa somo la domestic sience (sayansi kimu) sisi wengine
tulijifunza kule namna ya kuandaa chakula. Na kwanini wanafunzi hawana mashamba
ya shule,”alisema.
Mbunge wa
Viti Maalum (CCM) Anna Lupembe aliunga mkono kauli ya Sitta ambaye alitaka
wataalam wa lishe kutembea katika halmashauri kwa ajili ya kutoa elimu ya lishe
bora.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Stanslaus Nyongo alisema suala la lishe
ni muhimu sana halifai kuchukuliwa kiwepesi.
Alitaka
suala la lishe na magonjwa ya kuambukizwa kupelekwa chini ya ofisi ya Waziri
Mkuu ili yaweze kuratibiwa kikamilifu.
Mkurugenzi
wa shirika hilo Neema Lugangira alisema udumavu unaotokana na lishe duni
unaleta unasababisha uwezo mdogo wa kufyonza virutubishi na uyeyushaji wa chakula.
Alitaja athari nyingine ni riski ya kupata magonjwa
mbalimbali hasa ya kuambukiza, kuugua mara kwa mara kwa mtu mmoja mmoja na kwa
familia, gharama kubwa ya matibabu.
“Ongezeko kwa kasi ya ugonjwa mfano Ukimwi kiwemo mama
mwenye Ukimwi kumuambukiza mtoto Ukimwi. Elimu duni haswa kwa vijana,”alisema.
Alisema udumavu unaweza kupunguza uwezo wa kufikiri wa mtu na upungufu wa madini
joto, unaweza kupunguza, kuzaa mtoto mwenye uzito pungufu na upungufu wa
wekundu wa damu
Mbunge wa
Viti Maalum (CCM) Dk Thea Ntara alishauri wataalam wa lishe nchini kufanya
utafiti wa vyakula vinavyoweza kumpatia mtu vitamin E.
Mbunge wa
Mkinga (CCM) Dustan Kitandula alisema fedha zinazotengwa na halmashauri kwa
ajili ya lishe zimekuwa hazitumiki katika shughuli iliyokusudiwa.
Alishauri
Serikali kutenga fedha za lishe katika bajeti kuu ya Serikali na kuziwekea uzio
badala ya utaratibu wa sasa wakuziachia halmashauri kupanga bajeti hiyo.
Mbunge wa
Iringa (CCM) Jesca Msambatavangu aliwataka wataalam wa lishe nchini kufanya
utafiti katika mbegu za asili zinazopatikana katika maeneo mbalimbali kwa ajili
ya kuboresha lishe.
Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Agri Thamani na Mbunge Neema Lugangira alisisitiza kuwa
lengo la Semina ya Lishe Bora kwa Wabunge ni kuhakikisha kwamba Ajenda
ya Lishe Bora inakuwa ya kipaumbele, inazungumziwa na inafuatiliwa
kuanzia ndani ya Bunge hadi kwenye Mabaraza ya Madiwani ngazi ya Wilaya
ambapo Kila Mbunge ni Diwani katika Wilaya yake.
Hata hivyo alisema kwamba ni matumaini
yake kwamba ndani ya Miaka 5 hii 2020-2025 Tanzania itapata Mageuzi
Makubwa Katika Suala zima la Lishe Bora na kupunguza kwa kiasi kubwa
Udumavu na aina zote za Utapiamlo nchini