Mkuu wa Shirika, mwanachama wa Jumuiya ya Kijiografia ya Urusi, Yuri Korobov anasema “Kwanza, tumejipanga kufanya kazi katika miradi ya mazingira. Hii ni kati ya Urusi na Tanzania, tatizo la ukataji miti hovyo ni baya. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakikata misitu ya asili iliyoenea kwenye maeneo mbalimbali.
“Tanzania inakabiliwa na matatizo kadhaa ya mazingira, hiyo imekuwa ikiathiri maendeleo ya mazingira kwa kiasi kikubwa.
“Tatizo kubwa linaloikabili Tanzania ni uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa mazingira, kukosa maji safi katika baadhi ya maeneo ya mjini na vijijini na upoteaji wa wanyamapori,”.
Jumuiya ya Urafiki ya Urusi inajipanga kufanya kazi na mashirika kama Baraza la Kitaifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambalo lina jukumu la kuishauri serikali juu ya mambo yote yanayohusiana na mazingira.
Korobov alisema pia wataangalia changamoto zingine ambazo zimekuwa kikwazo katika kuathiri mazingira Tanzania.
Kuangalia migodi iliyotelekezwa, ambayo haihifadhiwi vizuri baada ya kuchimba madini, ikitoa gesi hatari za kemikali ambazo husababisha uharibifu wa udongo.
Ukataji miti kwa wingi
“Shida zote hapo juu zinaweza kupunguzwa kwa gharama ya teknolojia zilizopo nchini Urusi. Ndio sababu tumepanga kufanya mafunzo ya pamoja na kubadilishana wataalamu – wanamazingira, wahandisi, wakemia na wanaojitolea,” alisema Korobov.
Jumuiya ya Urafiki ya Urusi na Tanzania zinatarajiwa kutia saini makubaliano yao ya kwanza na Jumuiya ya Urafiki ya Tanzania mwishoni mwa Juni 2021. Kama sehemu ya makubaliano, vyama vitaunda baraza la biashara, ambalo litajumuisha watumishi wa umma na wajasiriamali.
“Kwa pamoja tutafanya kazi na kutekeleza uelewa wa jinsi miradi inapaswa kutekelezwa kila mahali, hata katika miradi ya kibiashara, ambayo tutashiriki kama washauri na kutoa msaada wa habari, kuna mwelekeo wa mazingira,” alisema Korobov.
Aliongeza, shirika limepanga kutekeleza miradi mingine kadhaa, ambapo miongoni mwao ni uundaji wa jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi kati ya biashara ya Tanzania na Urusi, kufanyika kwa jukwaa la uchumi lenye kaulimbiu ya kuvutia uwekezaji wa pande zote, utayarishaji wa mipango ya elimu kwa wanafunzi na vijana wa Urusi na Tanzania, ushirikiano katika maendeleo ya sekta ya kilimo ya nchi zote mbili, na pia utekelezaji wa mipango salama ya utalii, ubadilishaji wa kitamaduni.
Jumuiya ya Urafiki na Tanzania ilianzishwa nchini Urusi Aprili 2021 na kikundi cha watu maarufu na wajasiriamali kukuza miradi ya mazingira katika kiwango cha kimataifa.
Mwaka 2019, Sochi iliandaa mkutano wa kwanza wa uchumi wa Urusi na Afrika, ambao ulisababisha tamko lenye malengo ya maendeleo zaidi ya ushirikiano wa Urusi na Afrika katika nyanja za siasa, usalama, uchumi, sayansi, teknolojia na tamaduni.
Mkutano wa pili wa Urusi na Afrika umepangwa kufanyika mwaka 2022.
Tunatarajia urafiki wenye matunda kati ya Urusi na Tanzania kuelekea nchi rafiki ya mazingira na ushirikiano utakaoendelea.