Mhandisi Idara ya Uendeshaji wa UCSAF Shirikisho Mpunji akiongea na waandishi wa habari katika semina iliyotolewa na mkofuko huo kwa watoa huduma za mawasiliano kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya watoa huduma za mawasiliano kanda ya kaskazini wakisikiliza jambo katika semina waliyopewa na mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) semina iliyofanyika mkoani Arusha.
*******************************
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Mfuko wa mawasiliano kwa wote(UCSAF) uliyo chini ya wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari umewajengea uelewa watoa huduma za mawasiliano kanda ya Kaskazini kwa kueleza wajibu wa mfuko huo pamoja na wajibu wa watoa huduma hao kwa mfuko.
Akiongea na waandishi wa habari mhandisi Idara ya Uendeshaji wa UCSAF Shirikisho Mpunji alisema kuwa wajibu wa mfuko huo ni pamoja na kubainisha maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku kutoka katika mfuko huo, kuweka vigezo vya maeneo ya utambuzi katika vijiji vinavyohitataji na haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu ya kutokuwa na mvuto wa kibiashara na kuanzisha mfumo madhubuti wa usimamizi wa fedha.
Alisema kuwa kazi nyingine ya mfuko ni kuweka vigezo sahihi vya utoaji ruzuku kwajili ya kupeleka huduma katika maeneo yaliyoainishwa, kufanya tafiti na kufiatilia maendeleo ya mawasiliano maeneo ya vijijini na yale yasiyo na mvuto wa kibiashara, kuishauri TCRA, kusimamia kisheria mikataba ya utekelezaji wa majukumu ya ya utoaji huduma kwa wote pamoja na kupendeleza sera madhubuti za mfuko kwa waziri wa sekta ya mawasiliano.
Aidha mhandishi Shirikisho alieleza kuwa malengo ya mfuko huo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mjini yenye mawasiliano hafifu, kuhamasisha sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma ya mawasiliano kwa wote, kuhamasisha maendeleo ya kijamiina kiuchumi maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu pamoja na kutengeneza mfumo kwaajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji wa soko la kiushindani.
“Lengo letu lingine ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inapatikana vijijini na sehemu za mjini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu,”Alisema Shirikisho.
Pia alisema kuwa hadi sasa mfuko huo umetekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya mawasiliano ya simu za mkononi vijijini kwa kusaini mikataba ya kufikisha mawasiliano katika kata 1057 zenye vijiji 3292 na wakazi 12,981,164 ambapo kata 705 zenye vijiji 2550 na wakazi zaidi ya milioni 8 tayari imeshakamika.
Alifafanua kuwa pia mfuko umeweza kuanzisha vituo vya TEHAMA ambavyo vitaleta manufaa makubwa kwa wananchi, mradi wa kuunganisha shule za serikali 711 na mtandao wa internet pamoja na mradi wa wasichana na TEHAMA wa kutoa mafunzo ya kuandika programu rahisi za kompyuta kwa wasichana 690 na kuwashindanisha.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mkutano huo akiwemo Odero Charles ambaye ni mmliki wa watetezi Tv wanaishukuru mfuko huo kwani unatekeleza haki ya msingi ya kupata na kutoa taarifa kwa kuzifikia sehemu ambazo hazifikiki ambapo wao kama wadau wanataka mawasiliano yasiwe ya kutafuta kwa tochi.
Amos Ngosha mmiliki kutoka voice of Afrika alisema kuwa kuna haja ya mfuko huo kuvitumia vyombo vya habari kujitangaza ili wafahamike zaidi lakini pia kuionyesha jamii fursa zilizopo katika mfuko huo.
Naye Maimuna Msangi kutoka Pangani radio alisema kuwa wao kama wadau wana nafasi kubwa ya kunufaika na mfuko huo kwa kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo vitendea kazi ili jamii iweze kupata habari za kweli na uhakika.