Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka,akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mahusiano na Masoko wa Chuo cha Takwimu na Mashariki mwa Afrika Bw.Eusebius Mwisongo mara baada ya kutembelea banda hilo katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.kushoto ni Afisa Udahili wa chuo Hicho Samuel Marandu.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akiweka saini katika kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (katikati) ni Afisa Mahusiano na Masoko wa Chuo hicho Bw.Eusebius Mwisongo katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.kushoto kwake ni Afisa Udahili ,Samuel Marandu
Afisa Udahili wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika Samuel Marandu akitoa elimu kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato walipotembelea banda la Chuo hicho katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika mara baada ya kutembelea banda hilo maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Chuo hicho kinatoa Kozi Zifuatazo kwa mwaka wa masomo 2021/2022
1) Certificate in Statistics
2) Diploma in Statistics
3) Bachelor Degree in Official Statistics
4) Post graduate Diploma in Official Statistics
5) Postgraduate Diploma in Agriculture Statistics
6) Master of Official Statistics
7) Master of Science in Agriculture Statistics (MAS)