Mkurugenzi wa Tafiti ya Mazingira Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Menan Jangu, akifungua rasmi mafuzo ya Maafisa Mazingira wa NEMC ili kufuzu katika Ukaguzi wa Mazigira, yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma. mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuazia 30/5/2021 mpaka 2/6/2021. Kwanza kushoto Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Utekelezaji na Uzingatiaji wa Mazingira NEMC Muhandisi Redempta Samwel pamoja na Mwanasheria wa NEMC Bwa. Wanjara Jandwa
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo wakisikiliza kwa makini maelekezo ya Mkurugenzi wa Tafiti ya Mazingira Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Menan Jangu (hayupo pichani).
Mkurugenzi wa Tafiti ya Mazingira Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Menani Jangu, akiwa katika Picha ya Pamoja na washiriki wa mafuzo ya Ukaguzi wa Mazingira jijini Dodoma.
******************************
Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC), ya andaa mafunzo kwa Maafisa Mazingira kwa lengo la kukuza uelewa ili kufuzu kuwa wakaguzi wa mazingira ambao mwisho wa mafunzo hayo watapewa vitambulisho kuwa wakaguzi rasmi. Vitambulisho hivyo vitatolewa na Waziri mwenye dhamana ya mazingira nchini. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Menan Jangu, amesema kuwa, lengo la kufanya mafunzo hayo ni kuhakikisha kuwa NEMC inaongeza uwezo wa kusimamia mazingira kulingana na Sheria ya Mazingira na kukuza uelewa wa namna ya kusimamia mazingira kwenye jamii yetu.
Ameedelea kusema kuwa kuchaguliwa kuwa Mkaguzi wa Mazingira ni cheo kikubwa hivyo kila mtu ambaye amepata fursa hii ya kujifunza na kuweza kupewa kitambulisho kama Mkaguzi wa Mazingira ana dhamana kubwa katika kusimamia Uhifadhi wa Mazingira Nchini.
“Mkaguzi wa Mazingira anatakiwa kutumia mbinu rafiki katika kuelimisha au kuelekeza mtu ili aweze kutekeleza maelekezo anayopewa kulingana na sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Pale ninaposema kuwa Mkaguzi wa Mazingira ni cheo kikubwa hii ni kutokana na kifungu cha 182 cha Sheria ya Mazingira ambacho kinampa dhamana Waziri mwenye dhamana ya Mazingira kuteua Mkaguzi wa Mazingira na tutambue kuwa unapoteuliwa unakuwa mwakilishi wa Waziri katika kusimamia mazingira kwenye jamii inayokuzunguka. Hivyo kila mtu atumie nafasi hii kujifunza na kujua jukumu alilonalo ni kubwa.”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Utekelezaji na Uzingatiaji wa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira (NEMC) Muhandisi Redempta Samwel, amesema kuwa anaamini baada ya kumaliza mafuzo hayo kila mtu atakuwa amejifunza vya kutosha na atakuwa mfano mzuri katika jamii katika kutekeleza wajibu wake kikamilifu katika usimamizi wa mazingira.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia 31/5/2021 mpaka 2/6/2021.