Baadhi ya wanafunzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga wakiwa katika maandamano huku wakipiga saluti kwa mgeni rasmi hayupo picha wakati wa ufunguzi wa michuano ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi i (UMITASHUMTA) ngazi ya Mkoa wa Pwani yamefunguliwa rasmi katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Edrward Mwakipesile ambaye alikuwa ni mgeni rasmi katika ufunguzi huo wa mashindano akizungumza na wanafunzi, walimu, maaafisa michezo pamoja na maafisa utamaduni.
Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta akitoa salamu zake kwa mgeni rasmi kuhusiana na na mashindano hayo ya UMITASHUMTA ngazi ya Mkoa wa Pwani.
Mmoja wa maafisa elimu kutoka Halmashauri ya Chalinze akizungmza neno wakati wa halfa ya ufunguzi huo.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
***********************************
NA VICTOR MASANGU, PWANI
MASHINDANO ya umoja wa michezo na taaluma kwa shule za msingi i (UMITASHUMTA) ngazi ya Mkoa wa Pwani yamefunguliwa leo rasmi katika viwanja vya shirika la elimu Kibaha kwa kuwashirikisha wanamichezo wapatoa 637 kutoka halmashauri zote tisa na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja , viongozi wa vyama vya michezo pamoja na walimu.
Akifungua mashindano hayo Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Edrward Mwakipesile ambaye alikuwa ni mgeni rasmi amewataka wanamichezo hao ambao ni wanafunzi wa shule za msingi kutoka halmashauri mbali mbali kuhakikisha kwamba wanakuwa na nidhamu katika kipindi chote cha michuano hiyo.
Aidha aliwahimiza kucheza kwa juhudi zote na kuonyesha vipaji vyao ambavyo vitaweza kuwafanya kuweza kuchaguliwa katika suala zima la kuunda kikosi cha timu ya Mkoa mabcho kinatarajiwa kwenda kushiriki katika michuano ya ngazi ya Taifa mwezi wa sita Mkoani Mtwara.
“Kitu kikubwa kinachotakiwa ni kuhakikisha kwamba pamoja na kuwa nyinyi ni wanafunzi lakini ni wana mchezo hivyo katika kipindi hiki chote cha mashindano haya ambayo yameandaliwa maalumu kwa ajili ya kuweza kuchagua timu ya Mkoa wa Pwani ili kiweze kushiriki katika michuano ya Kitaifa mimi ninawaomba wachezaji wote ambao watachaguliwa kucheza kwa bidii pamoja na kujituma wakati wote,”alisema Mwakipesile.
Pia aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanatumia fursa za michezo mbali mbali katika kutimiza ndoto zao ikiwemo kujipatia ajira kupitia nyaja ya michezo katika siku za usoni na kuwaomba kuzingatia taratibu na sheria zote ambazo zinatumika katika michezo hiyo.
Mwakipesile pia hakusita kuwaomba walimu pamoja na maafisa michezo kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kuhakikisha wanafanya uteuzi wa kuchagua kikosi bora amabcho kitaweza kuuuletea heshima Mkoa wa Pwani katika michuano hiyo ngazi ya Taifa kwani anatambua kutakuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na Mikoa mbali mbali kujiandaa vya kutosha.
Katika hatua nyingine Mwakipesile aliwataka waamuzi mbali mbali amabo wanachezesha katika michezo tofauti kuzingatia miongozo yote n ataratibu ikiwemo sambamba na kuhakikisha wanatenda haki bila ya kuwa na upendeleo wowote lengo ikiwa ni kupata wawakilishi ambao wana uwezo katika kutimiza wajibu wao,
Aidha alisema kwamba serikali ya Mkoa wa Pwani itaendelea kushirikiana bega kwa began a walimu wa michezo, maafisa michezo pamoja na maafisa utamaduni katika kuleta mabadilio chanya ya kukuza vipaji kwa wanafunzi mashuleni na kuwahimiza waweke mikakati ya kwenda kujiendeleza zaidi katika vyuo ambavyo vimetengwa kwa ajili ya kufundisha micheoz.
Kwa Upande wake Kaimu Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani Hildegard Makundi alisema kwamba katika mashindano hayo yameweza kuwajumisha wanafunzi wapatao 637 kutoka katika halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani.
Alifafanua kwamba katika mashindano hayo michezo mbali mbali itachezwa ikiwemo mchezo wa soka, Riadha, netiboli, kurusha tufe pamoja na mingineyo na kwamba baada ya hapo watachaguliwa wachezaji 86 ambao wataunda kikosi cha Mkoa wa Pwani kwa ajili yakwenda kushiriki katika hatua ya ngazi ya Taifa Mkoani Mtwara.
“Leo ndio tumefungua rasmi mashindano yetu haya kwa shule mmbali mbali za msingi na kwamba kwa sasa tuna jumla ya wanamichezo wapatao 637 lakini baada ya kumalizika kwa mchujo ambao utafanywa na walimu tutabakisha wachezaji wapatao 86 tu ambao ndio sasa wanauwakailisha Mkoa wetu wa Pwani katika mashindano ya Taifa,”alisema Kaimu huyo.
Naye Afisa michezo wa Mkoa wa Pwani Grace Buleta alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha kwamba katika msimu huu wa mwaka wa 2021 wanafanya vizuri katika michuano hiyo ngazi ya Taifa na kuwaomba wadau wa michezo mbali mbali kutoa sapoti na ushirikiano wakati wa kipindi chote timu itakapokuwa katika Mkoani Mtwara kwa lengo la kurudi na ubingwa.