Msajili wa Bodi ya maziwa nchini Dk. George Msalya,akizungumz na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza maadhimisho ya wiki ya Maziwa kitaifa yatafanyika Mkoani Tanga.
……………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Msajili wa Bodi ya Maziwa nchini Dkt.George Msalya amesema karibu bilioni 22 zimekua zikitumika katika uagizaji wa maziwa kutoka Nje na kuingia nchini kupitia taasisi zake .
Hayo ameyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya Maziwa yatafanyika June 1 hadi 4 mwaka 2021,Mkoani Tanga amesema kuwa uagizaji maziwa kutoka nje ya nchi umekuwa ukiliumiza soko la ndani.
Dk.Msalya amesema kuwa suala la unywaji maziwa kwa watanzania bado linaokena kutokua na hamasa licha ya serikali kutumia juhudi kubwa katika uhamasishaji wa matumizi ya maziwa
“Bado uelewa ni mdogo mtu badala ya kunywa maziwa wanakwenda baa kunywa pombe wakati maziwa ni muhimu kuliko hiyo pombe”amesema
Hata hivyo Dk.Msalya amewataka watanzania kuwa na uzalendo wa kutumia bidhaa za ndani za maziwa ili kuwainua wafugaji, wasindikaji na wachakataji wa bidhaa hiyo kwani zipo bidhaa nzuri za maziwa zinazotengenezwa nchini.
Dk.Msalya amesema kuwa nchi yetu bado ina uzalishaji mdogo wa maziwa kwani inazalisha Lita bilioni 3.4 ambapo ukigawanya kwa idadi ya watanzania, kila mtu atakunywa wastani wa Lita 50 tu kwa mwaka.
Amesisitiza kuwa mujibu wa wataalamu wa Afya mtu anatakiwa kunywa maziwa Lita 200 Kwa mwaka hivyo bado kuna uhitaji mkubwa wa uzalishaji zaidi wa maziwa kwani ni kinywaji muhimu Kwa Afya ya binadamu.
Dk.Msalya amesema kuwa Maziwa ni biashara nzuri endapo yatatunzwa na kuhifadhiwa vizuri ndio maana kuna makampuni kama Asasi na Tangafresh ambayo yamekuwa yakifanya biashara hiyo ya uuzaji na ununuaji wa maziwa.
“Maziwa ni mlo kamili kwani unaweza usile ugali,maji na vyakula vinginevyo kwasababu yana protini ya kutosha,hivyo watanzania wanapaswa kunywa maziwa kwasababu ya afya zao kwani ni muhimu”amesema
Amesema kuwa maadhimisho haya yanafanyika tanga kwasababu ni mkoa ambao unazalisha maziwa kwa wingi,lakini pia kuna chama cha uzalishaji wa maziwa(TDCU),vilevile biashara ya maziwa imeshika kasi hivyo wadau wengi watajifunza.
“Maziwa yanachangia kwa ukuaji wa uchumi,ni mlo na muhimu kwa afya,lakini pia uzalishaji mdogo unachangia uingizaji wa maziwa kutoka nje ya nchi kama vile ya unga na mengineyo”amesema Dkt. Msalya.
Pamoja na hayo amewaasa watanzania kunywa maziwa yaliyo sindikwa kwani kuna uwezekano wa kukaa muda mrefu,nakuwataka kuwaunga mkono wafanyabiashara waliopo nchini.
Aidha amesema kuwa uhamasishaji wa unywaji wa maziwa umechangia kuongezeka kwa maziwa na hata mifugo,lakinipia imahamasisha kuongezeka kwa ulaji na usindikaji kwani tulikuwa chini ya lita 50 lakini kwa sasa tupo juu ya 50ambapo kwa sasa sekta ya mifugo inachangia pato la taifa kwa asilimia 7.
Aidha Dkt.Msalya amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2005 Tanzania imepiga hatua katika uzalishaji wa maziwa kwani mwaka 2015 kushuka chini wastani kila mtu alikuwa anakunywa Lita 40 Hadi 45.
Hivyo kufikia mwaka 2015 hadi 2021 kila mtu anakunywa maziwa Lita 50 kwa mwaka ambapo katika pato la Taifa maziwa yanachangia kwa asilimia 30 huku katika sekta ya mifugo ikichangia Kwa asilimia 7.
Amesema kuwa maadhimisho hayo yatalenga katika kufanya tafiti kuhusu tasnia ya maziwa, kujifunza namna ya kufuga ng’ombe bora wa maziwa na kugawa maziwa katika makundi mahitaji kama wagonjwa katika hospitali mnalimbali.
Wiki ya Maziwa Duniani duniani ilianzishwa baada ya kugundua unywaji ni mdogo na sasa kuamua kuipigia chapuo ili kuyapa kipaumbele ili kuboresha afya za wananchi.
Kauli Mbiu : Kunywa Maziwa ya Kwetu, Ongeza Uzalishaji na Usindikaji, Kazi Iendelee