Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe,akipata maelezo kutoka kwa Mhadhiri na Mratibu wa Kituo cha Msaada wa Kisheria, Dk Natujwa Mvungi mara baada ya kutembelea banda la Law School of Tanzania wakati maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe,akitoa maelezo mara ya kutembelea banda la Law School of Tanzania wakati maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. James Mdoe,akiweka saini katika kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Law School of Tanzania katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka akiweka saini katika kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Law School of Tanzania katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.kulia kwake ni Afisa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Taasisi hiyo Scholastica Njozi
…………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mhadhiri wa Taasisi ya Mafunzo ya uanasheria kwa Vitendo Tanzania Dk Natujwa Mvungi,amesema kuwa wanatarajia kuanzisha kozi mpya ya wasaidizi wa sheria
Hayo ameyasema wakati akizngumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya pili ya elimu ya mafunzo na ufundi yaliyoandaliwa na NACTE kwa kushirikiana na Taasisi ya sekta binafsi (TPSF) yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Amesema kuwa kwa sasa wako katika hatua za mwisho za uanzishaji kozi hiyo ambayo matarajio ni kuwa ianze Septemba mwaka huu.
“ Kabla ya sheria mpya, wasaidizi wa sheria walikuwa wakipewa mafunzo ya kuwajengea uwezo na taasisi mbalimbali, Lakini kwa sasa wanatambulika Kisheria na ndio maana tukaona tuanzishe kozi hii.
”Amesema kozi hiyo ambayo itatolewa katika ngazi ya cheti itafundishwa kwa mwaka mmoja na itakuwa imesajiliwa chini ya Baraza la Vyuo vya Ufundi Tanzania(NACTE).“
Katika maonyesho haya tumekuja kuwaeleza wananchi na wakazi wa Dodoma tunaanzisha kozi mpya ya wasaidizi wa sheria ambao kwa sasa wanatambulika chini ya Sheria ya Usajili wa Sheria.
”Aidha Dk Mvungi amesema kuwa Law School ina kitengo cha kutoa Msaada wa kisheria bure kwa wananchi wasiokuwa na uwezo wa kulipa gharama za mawakili.
“ Kwa sasa tuko Dar es Salaam lakini tunafanya kazi na taasisi mbalimbali kama Tanganyika Law Society katika kusaidia wananchi kwa kutoa huduma za Kisheria bure.amesema ”Dk Mvungi
Hata hivyo amesema kuwa huduma ambayo imelenga kuwasaidia wananchi wasio na uwezo wa kifedha, na tuna vigezo vyetu vya kuwatambua na Sheria inatuongoza.
Na kwa tathimini inaonyesha wananchi wengi waliokuja kupata huduma kwetu Ni wale wenye mashauri ya ardhi, mirathi na ndoa.
”Law School inatoa mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kwa wahitimu wote wa Shahada ya sheria kutoka vyuo vinavyotambulika na serikali wanaotarajia kufanya kazi kama wakili binafsi au katika utumishi nchini.