Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo (wa tatu kushoto) pamoja na viongozi mbalimbali akiongoza matembezi ya hiyari kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021 ambapo alimuwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akizungumza na wananchi katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga akitoa neno la utangulizi wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la Medeli akizungumza wakati wa zoezi la upandaji miti ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.
Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na wananchi katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Selemani Jafo akipanda mti katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Hamad Chande akipanda mti katika eneo la Medeli kabla ya kuongoza zoezi la upandaji miti kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani jijini Dodoma leo Mei 29, 2021.
BALOZI wa Mazingira Nchini, Sakina AbdulMasoud ambaye pia ni Mwandishi wa Habari wa Uhuru Media Group, akishiriki zoezi la upandaji wa miti katika eneo la Medelii, jijini Dodoma leo Mei 29,2021
PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS
………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Selemani Jafo ameshiriki matembezi ya hiari ya upandaji miti ikiwa na lengo la kukiijanisha Dodoma kuelekea siku ya Mazingira Duniani huku akizitaka Halmshauri zote hapa nchini kupanda miti isiyopungua Milioni moja na laki tano kila mwaka .
Matembezi hayo yamefanyika leo Mei 29,2021 jijini Dodoma yaliyoanzia viwanja vya Bunge kuelekea eneo la Medeli ambapo shughuli ya upandaji miti imefanyika na kuhudhuriwa
“Lazima tulinde nchi yetu maeneo mengi leo hii yamegeuka kuwa jangwa ,mji huu ulikuwa hali yake mbaya sana siku za nyuma lakini sasa hv ukitoka juu kwenye ndege unaona dodoma ilivyo yakijani.
Hivyo Jafo ameziagiza Halmshauri zote hapa nchini kupanda miti isiyopungua Milioni moja na laki tano kila mwaka kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo husababisha madhara makubwa ikiwemo uharibifu wa Mazingira
“Hii ni siku maalumu kwa ajili ya upandaji wa miti,nawashukuru waliokubali wito wa kukubali kuja katika siku hii ya upandaji miti.
‘’upandaji huu wa miti unatusaidia sana kuhakikisha tunarekebisha mabadiliko ya tabia ya nchi’’amesema Jafo
Aidha,Jafo amesema katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi wameanzisha kampeni kabambe ya Usafi wa Mazingira na Utunzaji wa Mazingira kukabiliana na mabadiliko hayo.
Waziri Jafo amesema kutakuwa na kampeni ya mazingira na hii nikutokana na miti milioni 48 kila mwaka inakatwa hivyo kampeni hiyo itashikisha kila mtu na hii itakuja na mashindano ambayo itashindanisha,Mikoa Bora,halamashauri za wilaya,miji ,kata na vijiji ,vyuo, shule za msingi na sekondari na huku zawadi Kama magari zikitolewa kwa washindi.
“Tunataka Tanzania iwe ya mfano na kwenye taasisi za serikali tutapanda miti ya matunda,wakuu wa mikoa sasa tuhakikishe tunaenda kupanda miti katika maeneo yetu natamani kila mwanafunzi awe na miti mitatu na kuitunza jambo hili litakuwa jema Sana na suala hili lishuke hadi kwenye ngazi za familia”amesema
Hata hivyo amesema kuwa kampeni hii itazinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Philip Mpango June 5,2021 kwenye kilele cha siku ya mazingira Duniani, Waziri jafo aliteua Wajumbe 14 washauri pamoja na mabalozi 40 wa kampeni ya Mazingira yenye lengo la kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi shindani Duniani katika utunzaji wa Mazingira.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema kwenye ajenda kama Mkoa ni kuhakikisha kuwa Mazingira yanakuwa ya kijani.
“Kama viongozi wa Mkoa tutatekeleza maelekezo yatakayotolewa na Ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira na tuko tayari kwa jambo hili ambalo limeanzishwa na litatekelezeka’’ amesisitiza Mtaka
Naye Mbunge wa Jimbo la Dodoma Antony Peter Mavunde amesema kutokana na hali ya hewa ya Dodoma inahitaji muamko mkubwa wa upandaji miti huku akiahidi kuwa kampeni hiyo inafanikiwa kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.