Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (watatu kushoto) akikagua watuhumiwa waliokamatwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma baada ya kuanza Operesheni Maalumu ya Kudhibiti Uhalifu ambayo inaendelea mikoa yote nchini, lengo ikiwa kudhibiti na kukomesha matendo ya uhalifu,ziara hiyo ya kukagua wahalifu imefanyika jana, jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wapili kushoto) akimuhoji mmoja wa watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dodoma baada ya kuanza Operesheni Maalumu ya Kudhibiti Uhalifu ambayo inaendelea mikoa yote nchini, lengo ikiwa kudhibiti na kukomesha matendo ya uhalifu,ziara hiyo ya kukagua wahalifu imefanyika jana, jijini Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi,Gilles Muloto akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene pikipiki mbalimbali zilizokamatwa katika Operesheni Maalumu ya Kupambana na Uhalifu ambayo inafanyika nchi nzima lengo ikiwa ni kupambana na uhalifu.Ziara hiyo ya waziri imefanyika jana jijini Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa eneo la Chang’ombe ambao lengo la mkutano huo ni kuhimiza ulinzi shirikishi baada ya kuanza Operesheni Maalumu ya Kudhibiti Uhalifu ambayo inaendelea mikoa yote nchini, ikiwa na dhamira ya kudhibiti na kukomesha matendo ya uhalifu.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi