Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa NCAA (Usimamizi wa Wanyamapori na Nyanda za Malisho Vicktoria Shayo (Kulia) akielezea tathmini ya utekelezaji wa operesheni ya kufyeka mimea vamizi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Erasto Sima (Kushoto)
Baadhi ya Wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Taifa wakishiriki zoezi la kufyeka mimea vamizi katika Kreta ya Ngorongoro.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Erasto Sima (kushoto) akishiriki zoezi la kufyeka mimea vamizi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa NCAA. Bw. Novatus Magoma akiwaeleza wajumbe wa Umoja wa Wazazi Mkoa wa Arusha aina za Mimea vamizi na athari zake katika nyanda za malisho kwa wanyapamori.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi wa CCM Ndugu Erasto Sima (kulia) akiushukuru uongozi wa NCAA kwa kutekeleza operetioni ya kufyeka mimea vamizi na kuahidi kuwa Umoja huo uko tayari kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ili kumaliza tatizo la mimea vamizi ndani ya Hifadhi.
…………………………………………………………………
Na Kassim Nyaki-Ngorongoro Kreta Arusha
Viongozi wa umoja wa Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa wamefanya ziara katika Wilaya na Ngorongoro ambapo pamoja na mambo mengine wametumia ziara hiyo kufyeka mimea vamizi katika Kreta ya Ngorongoro.
Viongozi hao walioongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wazazi Taifa Ndugu Erasto Sima wametumia ziara hiyo kutembelea Kreta ya Ngorongoro kwa lengo la kuunga mkono Jitihada za hifadhi hiyo kwa kufyeka mimea vamizi.
“Tuko katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa ilani ya Chama chetu na suala la mazingira ni moja ya ajenda muhimu, katika kutekeleza hili tumeona haja ya kuunga mkono jitihada za uhifadhi na kuamua kuja kufyeka mimea vamizi ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na NCAA na wadau wengine wa uhifadhi, na tunafurahi kuwa kazi hii inaendelea vizuri katika kuangamiza mimea hii” alifafanua Sima.
Mwenyekiti wa Wazazi CCM Mkoa wa Arusha Hezron Mbise ameipongeza NCAA kwa jitihada za kuendeleza uhifadhi na kutunza nyanda za malisho katika eneo la kreta ya Ngorongoro ambalo limekuwa na mvuto mkubwa wa kitalii hasa kuwezesha watalii wanaotembelea Hifadhi hiyo kuona Wanyama mbalimbali na vivutio vingine katika eneo moja.
Kwa upande wake Kaimu Kamishna Msaidizi Mwandamizi (usimamizi wa Wanyamapaori na Nyanda za malisho) Vicktoria Shayo ameeleza kuwa operereshi hiyo iliyozinduliwa wiki mbili zilizopita imekuwa na manufaa makubwa ambapo hadi sasa zaidi ya ekari 600 sawa na hekta 238 zimeshafyekwa na Wanyama wameanza kurejea katika maeneo hayo yaliyokuwa yameathirika.
“Operation yetu kwa kiasi kikubwa imezaa matunda kwa kuwa tayari tumeshafyeka eneo kubwa, pamoja na vibarua zaidi ya 120 wanaofanya kazi hapa kila siku lakini tuna trekta tatu zinazofyeka, na pia tunaongeza trekta nyingine mbili ambazo zitafika mda wowote kuanzia sasa ili kuongeza nguvu ya kazi hii” aliongeza Shayo.