Kikosi cha timu ya Watumishi Chamwino ikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa CCM Samora.
Mchezaji wa timu ya Watumishi Chamwino akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa timu ya Iringa Veteran
Mchezaji wa timu ya Watumishi Chamwino akitafuta namna ya kumtoka mchezaji wa timu ya Iringa Veteran
Timu ya Watumishi Chamwino ikiwa katika picha ya pamoja kwenye uwanja wa CCM Samora
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Timu ya watumishi kutoka katika
halmashauri ya Chamwino jijini dodoma week and hii imefanya ziara ya kimichezo
mkoani Iringa na kucheza mechi ya mshikamano na timu mbili za veterans za
mkoani Iringa
Timu hiyo ya watumishi Chamwino
inayotoka katika Halmashauri ya Chamwino jijini Dodoma imeandaa mechi hizo za
kirafiki kwa lengo la kucheza michezo ya kirafiki na timu za mpira wa miguu na volleyball
za mkoani Iringa na kujenga mahusiano ya kirafiki na wachezaji wa timu hizo.
Timu hiyo ya watumishi wa
chamwino ilianza kwa mechi iliyowakutanisha na timu ya Iringa Veteran ambapo
hadi dakika tisini walikuwa wametoshana nguvu ya magoli mawili kwa mawili (2-2)
mchezo uliopigwa majira ya asubuhi katika dimba la CCM Samora mkoani Iringa.
Katika mchezo huo timu ya Iringa Veterani
ndio walikuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza mwishoni mwa kipindi cha kwanza
lililofungwa na Dr Idd ramadhani, hadi mapunziko walikuwa wanaogoza goli hilo
moja licha ya kuzidiwa eneo la kiungo na kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo
Dr. Idd Ramadhan aliwainua tena mashabiki kwa kuifungia timu yake goli la pili.
Kufuatia matoke hayo Timu ya
Watumishi Chamwino walirudi mchezoni na kufanikiwa kurudisha goli zote mbili
kupitia kwa mshambualiaji wao Costantine Rweyemamu katika kipindi cha pili.
Katika mchezo huo timu ya
Watumishi Chamwino walioneka kuwa timu bora kwenye eneo la kiungo na kuwasumbua
wapinzani ambao kwa kiasi kikubwa walilazimika kucheza mchezo wa kujihami zaidi
ili kuondoa aibu ya uwanja wa nyumbani kufungwa na wageni hao.
Akizungumza mara baada ya mchezo
nahodha wa timu ya Watumishi Chamwino Ally Komba alisema kuwa mchezo huo
ulikuwa mzuri kwa pande zote mbili kwa sababu walicheza kwa kutoa burudani kwa
mashabiki waliokuwa wamehudhulia mchezo huo.
Alisema kuwa wamekuwa Iringa kwa
lengo la kucheza michezo mingi ya kirafiki na kuongeza marafiki wengine wapya
ili kudumisha mshikamano kwa kuwa wamoja kwenye michezo na kufanya shughuli
nyingine za kimaendeleo.
“Tumepokelewa vizuri Iringa na
tumecheza mechi yetu ya kwanza huku tukiwa tunafurahia burudani ambayo
tuliitegemea hapa,kwa kweli tumefurahia mazingira ya Iringa toka tumefika jana
usiku hadi hii leo” alisema….
Kwa upande wake naohadha wa timu
ya Iringa Veterani Kelvin Kalinga alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu na wenye
ushindani mkubwa kutokana na timu zote mbili kuwa kwenye ubora uliosababisha
timu hizo kufungana goli mbili kwa mbili.
Alisema kuwa lengo la mchezo huo
ni kuongeza mshikamano baina wachezaji wa timu hizo ambao walikuwa
hawafahamiani kwa kiasi kikubwa.
Naye mratibu wa timu ya Watumishi
Chamwino Helen lisakafu alisema kuwa lengo la safari ya kutoka Halmashauri ya
Chamwino hadi Iringa ni kudumisha umoja na ushirikiano baina ya wachezaji
waliocheza zamani ambao wapo mikoa mingine.
Alisema kuwa wamekuwa
wakitembelea mikoa mingi kwa lengo la kuongeza marafiki na kuongeza ushirikiano
kwa wananchi na wachezaji wa timu ambazo wanaenda kucheza nazo.