Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani akizungumza wakati akifungua mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo ya mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje akielezea umuhimu wa mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya EWURA Bi.Victoria Elangwa,akizungumza wakati wa mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dk. Tito Mwinuka,akizungumza wakati mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa mafunzo ya mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani akikabidhi leseni kwa baadhi ya washiriki waliofanya vizuri mara baada ya kufungua mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiwa katika picha mbalimbali mara baada ya kufungua mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Nishati Dk.Medard Kalemani akiagana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje mara baada ya kufungua mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika leo Mei 28,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Nishati,Dk.Medard Kalemani amezitaka Taasisi mbalimbali za Serikali na watu binafsi ambao wanajenga majengo na wanaweka mifumo ya umeme maofisi au majumbani kuhakikisha wanatumia mafundi ambao wamesajiliwa na wana leseni ya kufanya kazi hiyo.
Akizungumza leo Mei 28 mwaka 2021,wakati akifungua mafunzo kwa mafundi wa umeme kuhusu sheria ya umeme ya mwaka 2008 na Kanuni za Ufungaji umeme za mwaka 2019 yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) yaliyofanyika jijini Dodoma.
Waziri Kalemani ameziomba Taasisi mbalimbali za Serikali na watu binafsi ambao wanajenga majengo na wanaweka mifumo ya umeme maofisi au majumbani kuhakikisha wanatumia mafundi ambao wamesajiliwa na wana leseni ya kufanya kazi hiyo.
Vilevile,ametoa wito kwa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuhakikisha kazi za mafundi waliosajiliwa ndizo zinazopokelewa na kukubalika ambapo amedai hali hiyo itasaidia kupunguza athari za ajali zinazotokana na mifumo isio mizuri ya uunganishaji wa umeme kwa wateja.
“Naagiza TANESCO kutumia kanzi data ya EWURA katika kupokea kazi za kandarasi za umeme na fundi yeyote mwenye leseni ya EWURA ana uhuru wa kufanya kazi popote Tanzania Bara,”amesema Waziri Kalemani.
Waziri Kalemani pia amewataka washiriki wa mafunzo hayo ni muhimu kwa washiriki hao kuzingatia weledi wa kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora,hivyo usalama wa mifumo ya umeme ni muhimu.
“Mafunzo haya pia yatumike kuwakumbusha umuhimu wa kuzingatia sheria kwa wale wasio leseni waweze kufuata utaratibu wa kupata leseni hizo,” amesema.
Amesema mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka katika Mikoa ya Kanda ya Kati ukizingatia mwelekezo wa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akieleza kila mtu kutimiza wajibu wake kwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Nchi.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Godfrey Chibulunje amesema tasnia ya wakandarasi inakabiliwa na changamoto za kuwa na mafundi wengi wasiosajiliwa huku wakifanya kazi bila usimamizi hivyo kazi nyingi kufanyika chini ya kiwango nap engine kusababisha ajali za moto muda mfupi mara baada ya kukamilika.
Ameitaja changamoto nyingine ni mafundi wengi kutokuwa na leseni ambao baadhi hutumia leseni mfu ambazo hawajazihuisha,baadhi ya mafundi kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Tanesco wasio waaminifu kuwafungia wateja hata kama kunaonekana dhahiri kuna udanganyifu katika nyaraka.
Mhandisi Chibulunje amezitaja changamoto zingine ni vifaa visivyokidhi viwango hali ambayo husababisha ajali za moto,kutokuwa na mfumo wa kuweka kumbukumbu,kukosekana wa kukagua miundombinu katika majengo.
Amesema ili kuleta nidhamu katika tasnia ya ufungaji wa mifumo ya umeme mamlaka inawataka mafundi wote wa umeme kuwa na leseni zinazotolewa na EWURA ambazo zimeboreshwa kulingana na mazingira ya sasa ya teknolojia.
“Makampuni ya umeme kuajiri au kuwasaidia mafundi wote kuwa na leseni sio kuwa na leseni moja tu kwa Msimamizi halafu wengine wote wasiwe nayo ili tu waendelee kufanya kazi kwao.Hakikisheni wakandarasi mnahakiki vyeti.Makampuni yaendeshwe kwa ujuzi.Mafundi wasiopata ajira za kudumu wajiunge katika vikundi vinavyotambulika kisheria ili waweze kufanya kazi,”amesema.