Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa kikao alichokiitisha jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko wa NHIF wanaotibiwa katika Hospitali hizo za Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi wa JKCI RN Robert Mallya.
Mkurugenzi wa Tiba na huduma za kitabibu kutoka mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Dkt. David Mwanesano akielezea kuhusu huduma za matibabu zinazolipiwa kwa wanachama wa mfuko huko wakati wa kikao kilichoitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa viongozi wa NHIF, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI),Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko huo wanaotibiwa katika Hospitali hizo za Taifa.
Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai akizungumza kuhusu huduma zinazolipiwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wanachama wake wanaotibiwa katika Hospitali hiyo wakati wa kikao kilichoitishwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa viongozi wa Taasisi hiyo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na NHIF kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazolipiwa na mfuko huo.
Mkurugenzi wa Tiba wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Hedinga Swai akiuomba mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuboresha huduma wanazozilipia kwa wanachama wake wanaotibiwa katika Hospitali hiyo wakati wa kikao kilichoitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa viongozi wa Hospitali hiyo, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na NHIF kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazolipiwa na mfuko huo. Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akichangia mada wakati wa kikao kilichoitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa viongozi wa Taasisi hiyo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko wa NHIF wanaotibiwa katika Hospitali hizo za Taifa.
Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga akiushukuru mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kuwalipa madai yao kwa wakati kwenye kikao kilichoitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa viongozi wa Taasisi hiyo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na NHIF kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko huo. Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja akizungumzia kuhusu umuhimu wa kuboresha kitita cha huduma zinazolipiwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa wanachama wake wakati wa kikao kilichoitishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima kwa viongozi wa Taasisi hiyo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na NHIF kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma hizo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakati wa kikao alichokiitisha kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa wanachama wa mfuko wa NHIF wanaotibiwa katika Hospitali hizo za Taifa. Kikao hicho kilifanyika jana katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na JKCI