Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akizungumza kwenye warsha ya wadau kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima vya maji nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza katika warsha ya wadau kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima vya maji nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji Dkt.George Lugomela,akielezea umuhimu wa warsha ya wadau kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima vya maji nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Baadhi ya Wachimbaji na Watafiti wa Maji nchini wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (hayupo pichani) katika warsha ya pamoja iliyofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi Water and Land Consult Centre Bw.Jonathan Mgaiwa,akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wenzake baada ya Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso kuzungumza kwenye warsha ya wadau kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima vya maji nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma.
WAZIRI wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amewataka wataalam na wadau wa maji kujikita katika tafiti za uchimbaji wa visima vya maji na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Kauli hiyo ametoa wakati akifungua warsha ya wadau wa maji kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima vya maji nchini iliyofanyika jijini Dodoma.
Mhe Aweso amesema kuwa watalamu wa maji wakitumia teknolojia bora na tafiti sahihi katika maeneo yao wanao uwezo wa kuchimba visima kwa siku moja na siyo kutumia muda mrefu kukamilisha visima .
Mhe.Aweso amesema kuwa hawa wachimbaji na watafiti ni wadau wetu wakubwa wa katika Wizara yetu, haiwezekani Wizara mwaka jana ilikua na mpango wa kujenga visima 542 lakini vilivyochimbwa hata 150 havifiki, hii maana yake Wakala wa Uchimbaji hamuwezi kufanya peke yenu washirikisheni hawa wadau
Mfano mwaka huu tuna Mpango wa kuchimba visima zaidi ya 1,000 niwaambie tu Wakala wa Uchimbaji toeni fursa kwa hawa wachimbaji, haiwezekani mnachimba kisima mwezi mzima bila sababu ya msingi, wapeni hawa wachimbaji muone kama hawatochimba kwa siku Moja,” Amesema Mhe.Aweso.
Hata hivyo amewaahidi wachimbaji hao kushughulikia changamoto zinazowakabili ikiwemo hiyo ya kuhakikisha wanalipwa madeni yao ya nyuma huku akiwataka kujenga umoja wao utakaowawezesha kuweza kuwasilisha changamoto zao Wizarani kwa haraka.
Kwa upande wake katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi Antony Sanga amesema kuna haja kuwa na sticker kwenye miradi kwa kampuni za maji zilizosajiliwa ili kubaini kampuni hewa.
”Wengi hawajasajiliwa ,mliosajiliwa ni wa hivyo kuna haja ya kuweka sticker katika kampuni mahali zinapotekeleza mradi wa maji hali hii itasaidia kuondoa changamoto kwenye utekelezaji wa miradi ya maji”amesema Mhandisi Sanga
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wamiliki wa kampuni 64 za uchimbaji visima nchini Jonatha Mgaiwa amesema watahakikisha wanasaidiana na serikali katika kutatua changamoto ya maji hapa nchini.
Warsha ya wadau wa maji kuhusu utafiti na uchimbaji wa visima vya maji imekutanisha zaidi ya kampuni 64 za uchimbaji visima nchini ambapo serikali ina mpango wa utekelezaji wa miradi ya maji 1527.