……………………………………………………….
Na Mwandishi wetu
Bendi kongwe ya muziki wa dansi nchini, The African Stars International ‘Twangapepeta’ kesho inatarajiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo pale itakapo kuwa akizindua albamu yake ya 14 katika Tamasha la Tanzania Music Regent Concert.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Afri Stars Entertainment Tanzania (ASET), Asha Baraka ‘The Iron Lady’ amesema tasha hilo litafanyika katika ukumbi mpya wa Break Point, Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Kinondoni.
“Tutasindikizwa na bendi ya Msondo na Tukuyu Band,”alisema Asha Baraka.
Amesema pia Watatopa tuzo kwa wasanii waliofanya kazi kubwa katika muziki wa dansi walio hai na waliokufa.
“Litakuwa tamasha kubwa lililosheheni burdani za kutoka. Twanga Pepeta ni bendi kongwe na tumejipanga kivuri kuhakikisha kila atakayeingia ukumbini atasuuzika moyo wake,”alisema
Mgeni rasmi katika tamasha hilo anatarajiwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omari Kumbilamoto.