Mwenyekiti wa wakuu wa taasisi zilizomo ndani ya wizara ya viwanda na biashara ambaye pia Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara, Prof.Emmanuel Mjema akizungumza na waandishi katika ziara yake mkoani Arusha.
Meneja wa SIDO Mkoa wa Arusha Bi.Nina Nchimbi akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na ugeni huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Tanzania,Silivester Mpanduji akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha.
*****************************
NA NAMNYAKKIVUYO, ARUSHA.
Mwenyekiti wa wakuu wa tasisi zilizomo ndani ya wizara ya viwanda na biashara ambaye pia ni mkuu wa chuo cha elimu ya Biashara, Prof.Emmanuel Mjema amesema kuwa kuna wajasiriamali wengi lakini hawana mawazo mapya ya kibiashara kutokana na wengi wao kuridhika na kile wanachokiuza.
Profesa Mjema aliyasema hayo wakati alipotembealea shirikala viwanda vidogo Arusha {SIDO} ambapo aliwataka wajasiriamali kufiria fursa za masoko hata nje ya Tanzania na hilo litawezekana kama wataboresha ubora wa bidhaa wanazotengeneza.
Alisema lengo la kutembelea SIDO pamoja na mashirika mengine ni kutambua fursa za mashirikiano baina ya taasisi hizo kwani zilipoanzishwa kila moja ilianzishwa kwa sheria yake lakini baadae wakaona kuna mambo mengi ambayo wanaweza tukashirikiana na kusaidiana katika kuboresha huduma tunazozitoa ama kutoa biadhaa bora zaidi kwa kutembeleana.
Alieleza kuwa katiaka tasisis walizozitembelea ikiwemo Taasisi ya TEMDO na CAMATEC wamekuta bidhaa nyingi zilizozalishwa lakini hazifahamiki nje ya taasisi zao jambo ambalo wameona ni eneo muhimu la kuwasaidia katika biashara pamoja na kuweka fursa za kibiashara kwa kuhakikisha wanatengeza mipango ya biashara zao.
Aidha alisema kuwa programu ya Kaizen ambayo inapatikana kwa ushirikiano wa CBE na SIDO itasaidia kupunguza gharama za uwezeshaji na kuongeza ubora wa ili wajasiriamali waweze kuwa na vifaa na bidhaa zenye ubora zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo Tanzania,Silivester Mpanduji alisema Shirika hilo la kuhudumia viwanda vidogo wanatoa mikopo kwa wajasiriamali ya shilingi Milioni 5 ambapo kwa kushirikiana na Benki ya CRDB wanatoa mkopo wa shilingi Milioni 10 hadi Milioni 50.
Alifafanua hivi karibuni wameanzisha mahusiano na benki ya Azania ,NSSF pamoja na VETA ambapo kwa sasa mtanzania anaweza kupata mkopo kati ya shilingi milioni 8 hadi milioni 50 na kwa wajasiriamali wanaokuwa wanaweza kupata mkopo kati ya shilingi milioni 50 hadi milioni 500 na wamefanya hivyo ili watanzania wengi waweze kuanzisha na kukuza viwanda vyao.
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Arusha Bi.Nina Nchimbi amesema kuwa ziara hiyo imewasaidia kuweza kuona fursa mbalimbali na kuweza kufanya nao kazi kwa karibu na kushirikiana ili kufikia Tanzania ya viwanda ya mafanikio.
“Changamoto kuu ambayo tunayo ni upatikanaji wa taarifa sahihi kwetu sisi kama taasisi lakini upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wajasiriamali ili kuweza kutambua na kuona taasisi zilizo chini ya wizara ya viwanda na biashara,”Alisema.